Nzokanhyilu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2007
- 1,078
- 104
Wakati Sisi Tunaendelea Kulala, Mafisadi Mambo Yao Yako Fresh Kabisaa, By The Time Madini Yanaisha Maisha Yao Na Wajukuu Wa Wajukuu Wao Yatakuwa Yana Uhakika Kabisaa, Kwa Hiyo Sidhani Kama Wanajali Na Hicho Kilio Chenu Cha Madini Yanaisha. Kwa Sababu Nasikia Kuna Fisadi Mmoja Mjukuu Wake Wa Miaka 4 Ana Mabilioni Kadhaa Benki, Huyo Atawaza Kujenga Miji Badala Ya Kujijengea Nyumba Zao? Na Inaweza Ikawa Sio Bongo Tuu Hata Nje Ya Nchi. Tusipoangalia Tutakuja Kuishia Kubaya Sana Huko Tunakoenda.
Kuhani,
Asante kwa kuweka article hiyo. Tena achana Ukweli ni kwamba, waafrika hatukai tukafikiria huko mbeleni tutafanya nini. Infact, ngoja nibaki Tanzania. Tanzania ni nchi 'inayoendelea' na tunahitaji nishati kwa kiwango kikubwa ili tuweze kuendelea. Personally, I have written off minerals. Hayo hayana maana kwetu. Hayana maana kwetu kwasababu madini ni cha mtoto ukifananisha na umuhimu wa nishati. Madini yangeweza kutumika kama means to another solution, lakini hata hatufikirii hivyo.
Ngoja nifananishe na ulaya kwenye ishu hii. Hapa UK, Holland, Germany, Scandinavia, mtu unaweza kuishi bila kutegemea gari (sanasana kwenye miji mikubwa). Kwa mfano, mimi nasafiri kutoka nyumbani mpaka kazini, door to door, nimepanda treni. Treni yenyewe inatumia umeme. Katika tripu yote hiyo, potentially, sijatumia umeme wa mafuta! Niachojaribu kusema ni kwamba, when push comes to shove, wazungu wakiamua kuweka magari pembeni sababu ya bei juu za mafuta, wanaweza. Yaani infrastructure yao iko tayari kubadili mwelekeo wa teknolojia. Wazungu walikuwa tayari, ilibidi wawe tayari tangu miaka ya 70, pale waarabu walipoleta za kuleta. They stepped up their game, ndio wakagundua mafuta huko North Sea, ndio wakagundua hadi jinsi ya kuchoma makaa kwa usafi zaidi na hadi uwezo wa kutengeneza gesi kutoka makaa. They read the problems ahead, wakajitayarisha. Nchi za ulaya ni 'ndogo' kutatua tatizo la transport. Nchi nzuri kuangalia itafanya nini kwenye tranposrt ni marekani. Hao bila magari, they are messed. USA itabidi wa-invest kwenye electrical transport, maana nchi ni likubwa, na kila mtu anataka atumie gari. Jinsi mafuta yalivyopanda bei, kuna watu siku hizi wanafanya kazi siku 3 tu ofisini, zingine nyumbani.
Aina mbalimbali za nishati zipo, na tutaendelea kuishi. Ugumu uko kwenye transport. There is nothing as cheap and efficient as oil when it comes to transport. Lakini muda ukifika kwa mafuta kuisha, teknolojia zingine zitakuwepo. Je wangapi wataweza kuhimili bei zake? Ukizingatia bei ya maisha ni ngumu kwa nchi zinazoendelea (au mbaya zaidi huko vijijini wanakochoma magogo = misitu). Wazungu huku hawana jua la kutosha. Kuna project kabambe inapigwa kati ya nchi za north Africa na nchi za ulaya. Wazungu, benki zao zinawekeza kwenye solar plants zitakazotapakaa north Africa, hao jamaa wa North wenyewe wanatoa ardhi tu. Project ikiisha, wanapata umeme locally kuwatosheleza, na mwingine unakwenda ulaya. mahesabu yaliyopigwa ni kwamba utatatua matatizo ya transport Ulaya. Hii inakuwa intergrated kwenye transport system ya kutumia umeme. Yaani mambo ya treni na tram yatatatuliwa!! Sasa chochote kingine kama bio-diesel, hydrogen or solar powered cars, teknolojia itakuwa imefika mbali na affordable kiasi kwamba watu watasahau oil. Lakini transport system yao itakuwa intergrated kiasi kwamba unaweza usihitaji gari kabisaaaa!! Panapo wasumbua wazungu sasa hivi ni air-transport tu!! Hapo mafuta ndo yanamuhimu, ila tatizo litatatuliwa with time.
Je, kama transport system yetu ni chokambaya mpaka sasa hivi, na hali ndivyo hivyo vijijini, tuna mipango gani na huko mbeleni? Hivi waafrika, watanzania tunajipenda kweli? Au siku zote sisi ni kufuata tu mkumbo na kununua teknolojia? Teknolojia gani tutanunua? Nuclear? Wazungu hiyo teknolojia watahakikisha wanashikiria na kukuuzia wewe tena umeme, sababu yao itakuwa kwamba nchi zetu ni unstable na teknolojia inaweza kutumika kigaidi. Can we blame them for considering us unstable? We have signs of, and we creating instability ourselves. We just dont like ourselves as africans, and when we do, we love ourselves for the wrong reasons and priorities!
Lusajo, it doesnt matter how much wealth someone has in Africa, things like this will catch up on the wealthy. You can not have wealth while basic things around you wont be functioning for the majority. You will be living in a melting pot of anger and potential violence from the have nots. Being excessively wealthy in an unstable society, where they know how you got your wealth, is fun only for a while. It does catch up. You only need one crazy person who is tired of the contrast, and that wealth will leave as quick as it came.
mimi nafikiri unaongelea vitu usivyovielewa na unachanganya mambo....
unajaribu kufananisha vitu visivyofanana kwanza moja mpaka sasa hivi hakuna suluhisho la mafuta hata huo umeme ambao unaendesha treni pia unategemea mafuta kwa namna moja au nyingine....
pili makaa ya mawe yalikuwa yanatumika kama chanzo cha nishati hata kabla mafuta hayajagunduliwa na si kwamba makaa ya mawe yameanza kutumika baada ya kuadimika kwa mafuta....
hao waingereza unaowaongela wana malighafi kubwa tuu ya mafuta huko bahari ya kaskazini na wanaitumia sana....
tatu kama kweli unaelewa ni nini maana ya solar power (ubadilishaji wa nishati ya jua kwenda umeme) na jinsi inavyofanya kazi sidhani kama ungeweza kusema kwamba madini ni cha MTOTO na nikihisi unamaanisha kwamba tuachane nao na kuwekeza kwenye solar power, sasa kwa taarifa yako ni ni kazi ngumu sana kuliko unavyofikiria huo mradi wa afrika kaskazini na ulaya ni ndoto kama zilivyo ndoto nyingi tuu dunia hii...
kuchimba madini chini ya ardhi kama makaa ya mawe kupakia ktk meli na kusafirisha ni rahisi zaidi na inaweza kuboresha maisha yetu haraka sana kama tukiweza kupambana na kuyatumia vema ambapo ndicho kitu mwanzisha hoja amekiongela...
hayo mambo ya kiteknojia kutoka ulaya na marekani achana nayo kwa sasa acha tupiganie madini ili yawe mikononi mwetu na hizo teknolojia tunaweza hata kununua ni rahisi zaidi...
Hoja hapa ilikuwa kuhusu madini yetu ambayo kutokana na mwanzisha hoja ni kwamba yatakwisha mwaka 2028, sasa kama ni kweli au si kweli hicho ni kitu kingine ila cha muhimu hapa ni kwamba ni nini tufanye ili tuweze kuokoa hilo kwani madini ni malighafi na kama unaelewa jinsi mambo yanavyokwenda ni rahisi zaidi kuweza kujenga uchumi kama ukiwa na malighafi asilia kuliko ukiwa huna sasa sisi tumejaliwa kuwa nayo kwa hiyo ni lazima tuweze kupigania ili itunufaishe, hizo nchi zote ulizoziorodhesha (isipokuwa moja ama mbili) zilijenga chumi zao kwa kutumia malighafi walizojaliwa na kutumia pesa hizo kuweza kuendeleza nyanja zingine.... marekani unayoijua wewe ingekuwa si marekani bila malighafi kwa taarifa yako na watu wengi hawalijui hili marekani ni moja ya nchi zilizojaliwa sana kuwa na malighafi nyingi sana duniani, mimi sijawahi kufika huko lakini nafahamu kwamba kuna majimbo megi tuu ambayo yalijengwa kwa malighafi pekee kama califonia isingekuwa califonia bila dhahabu, kanada, australia, n.k
Kwa hiyo kuweza kusema kwamba madini ni mtoto kutaka kutuposha na sidhani kama mawazo yako tunayahitajika ktk nchi yetu ni bora uyabakize huko huko uliko lkni usiyalete huku nyumbani.....
Utajiri wa waarabu ni wa kujitengeneza ila wetu sisi ni wa asili maana ikimaliza zaabu na vito vyengine basi ujue kuna Uranium ndio kwanza tunaitafutia vinu vya nuklia ,yaani ingawa nasikia kuna black market ya Uranium hapa Tz ,lakini naona ni majungu tu bado hawajapata mteja wa kuweza kuichokoa na kuifunga kwenye viloba ,maana ni dili la kimataifa ,kama tukitafuta mchimbuaji yaani aje temporari tu atuchokolee kilo moja ,kwa ajili ya kuichunguza basi tukimaliza kuichunguza tukaipiga bei ugali wake unaweza kuihudumia bajeti yetu ka kwa miaka 50 ijayo.Wacha waarabu watakuja kutufagilia majumbani na kufanya kazi za kuchunga mbuzi wetu na ng'ombe wa maziwa.
Bado unashindwa kuelewa kitu hapa.....Mkuu, wewe ndo hujui unachoongelea. Madini ni short term. Nchi yoyote dunia hii cha muhimu ni Energy, Water, Food, you control this, you are safe. Madini ni ya kupita. Ndio maana hata balozi wa Uholanzi, sijui kutoka nchi ya Scandinavia anawaambia, anayetegemea Tanzania iendelee ghafla kwasababu ya madini ana ndoto. You are not thinking big!!
Sasa hapo madini yanaisha 2028, wazungu wanachange gemu 2020. Nimetafuta na nimeipata project, bofya hapa TREC - Trans-Med Renewable Energy Cooperation
Makaa ya mawe yalikuwa yanatumika kwa kuchoma moja kwa moja, na ndio maana kuna miji imechoka huku ulaya kwa ajili ya uchafu wa makaa. Ikajulikana process inaitwa 'coal-gasification', hii inajulikana tangu zamani. Ila miaka ya 70s, wakaingia lab, wakaja na process inaitwa 'Integrated Gasification Combined Cycles' ambayo by-product yake ikawa Hydrogen, na ambayo inatumika kwenye magari. IGCC ni direct result ya matatizo ya mafuta in the 70s.
Kuhusu solar, ofcourse ni kazi ngumu, lakini ikiwa ngumu sio kwamba tusipange. Hayo madini yatakufikisha wapi wakati unachimba tu hata huendelezi nyanja zingine? Umeme ujanja wake ni ku-convert tu uweze ku-drive turbines, simple. Kuna solar plants California, Arizona (jangwani), we google utakutana nayo. Soma hiyo site ya TREC uone kiasi gani umeme watatengeza. California wanatumia technology tangu 70s/80s, direct result ya matatizo ya mafuta 70s ndugu yangu. 354MW of solar are added to the Southern California Grid, so what makes you think its not possible. Ishu ni kwamba teknolojia ipo tayari, ni expensive kwasababu oil is 'cheap'. Oil itapanda bei, na itaisha, eventually solar itakuwa cheaper!!
Sasa hayo madini unayolilia yamekusaidia nini? Yatakusaidia nini na hiyo 3% unayopata. Na Tanzania mafuta yanapatikana. In reality Wazungu wako desperate ndio maana hata kutafuta mafuta nchi kama Tanzania ni 'bei' rahisi sasa hivi. Mafuta/Gas ipo Tanzania na inajulikana for decades, only now its cheaper. And YES, the USA still has plenty of oil, lakini watazidi kununua sehemu nyingine, eventually they will have the last laugh. Watu wanaenda vitani kwa Energy, we kaa na madini unayoyalilia, hata hujui uyafanyie nini.
Unasema nikae hukuhuku, hujui mimi ninaweza kutoa mchango gani kwako na kwa nchi. Usilete ubishi wa kujifanya unajua nchi hata hamwezi kuongoza bila kua na mipango ya maana. Michango mingine mnataka, mawazo ya maendeleo hamtaki, we vipi wewe?
we kaa na kigari chako, weka kiyoyozi, ila subiri siku mafuta yaishe...sijui kama kutakuwa na vipanya wala nini, ndio utajua umuhimu wa transport. South Africa wenyewe, ni miji tu imeendelea, kwani walio vijijini vipi? Look at the bigger picture, sio unakaa tu Dar unafikiria ndio maisha yalivyo.
Bado unashindwa kuelewa kitu hapa.....
hakuna aliyekubishia kwamba madini hayaishi.... ninachokwambia ni kwamba suluhisho unalotoa weye ni GUMU SANA KULIFIKIA UKILINGANISHA NA KAMA TUNGEWEZA KUWEKEZA KTK MADINI.... sasa hauwezi kuanza kuongelea Solar power ktk nchi yetu wakati hata utafiti wa kuweza kuzalisha chakula cha kutosha bado hatujafikia sasa tunawezaje leo kuanza kufikiria kujenga solar power plant? na ndio maana nikwambia kwamba kama unamaanisha unachoshauri basi hauelewi unachokisema....
NINACHOSEMA NI KWAMBA NI LAZIMA TUPIGANIE MADINI YALIYOPO ILI TUWEZE KUFAIDIKA NAYO, SASA SIONI KIGUMU KIPO WAPI KWAKO KUELEWA HILO, NA NDIO KITU HASA MWANZISHA HOJA ANACHOZUNGUMZIA KWAMBA MADINI YETU YATAKWISHA SASA TUFANYE KILA TUWEZALO ILI YATUNUFAISHE NA KUTUMIA FEDHA TUTAKAZOPATA KUWEKEZA SEHEMU NYINGINE KWANI NI RAHISI KWA NJIA HIYO KULIKO NJIA UNAYOPENDEKEZA WEWE,....
Unachonishangaza mimi ni wewe kuanza kuongelea mambo ya solar plant wakati tz bado tunaweza pia kutumia maji yaliyotuzunguka kupata umeme....
tumezungukwa na mito na maziwa na bado maji masafi ya kunywa hatuna na unaanza kuongelea mambo ya solar plant hapo ndipo pointi yako siipati....
Usizugwe na hayo unayosoma kwenye google mimi nakwambia hata hayo masolar plant bei yake ipo juu sana kama unataka kuelewa angalia bei tuu ya solar panel ndogo labda hilo litaamsha ubongo kidogo ktk hilo.....
vile vile kama kweli unaelewa jinsi ya kujenga solar plant bado pia unahitaji gesi na vinginevyo ili plant iweze kufanya kazi kikamilifu....
sasa tumejenga solar plant labda singida halafu inabidi tupeleka mikoa ya jirani unajua bei yake lakini...Je hauoni kama ni rahisi kuwekeza kwenye maporomoko ya maji tuliyonayo mengi na kupata umeme wa kutosha....
ndio nikakwambia unaongelea vitu usivyovielewa na kulinganisha visivyolingana....
na ukiangalia nchi zote zinazofanya hiyo miradi ni kwamba serikali zinatoa pesa nyingi sana....
sasa sisi bajeti ni dola bilion 6 tunaweza kweli kuwekeza kwenye solar plant.....
hapa cha muhimu ni kupiga kuuwa na kuokoa madini yetu ndio njia pekee kwa sasa hayo mengine ni ndoto tuu....
PIGA UA NI LAZIMA MADINI YETU YABAKI KUTUSAIDIA NA HICHO NDICHO KITU CHA KUPIGANIA NA SIO SOLAR PLANT............