Mikate imeadimika kabisa huko Kilimanjaro. Sababu wingi wa watu walioenda kusherekea Krismasi na Mwaka mpya

Mikate imeadimika kabisa huko Kilimanjaro. Sababu wingi wa watu walioenda kusherekea Krismasi na Mwaka mpya

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Hii sasa ni balaa!
Mkate umekuwa dili huko Kilimanjaro
=================
Kufuatia wingi wa watu waliokuja kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya mkoani Kilimanjaro, bidhaa aina ya mkate imeadimika katika maduka makubwa (supermarkets) mjini Moshi na kusababisha adha kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.

Bidhaa hiyo ambayo hutumiwa na familia nyingi imekuwa adimu kuanzia jioni ya leo, Desemba 24, 2024 na baadhi ya watu waliofika katika maduka hayo hawakupata mikate.

Hata hivyo, Mwananchi Digital imepita katikati ya mji na kushuhudia maduka hayo yakiwa hayana mikate hali itakayowalazimu walaji hao kutumia njia mbadala.

Wakizungumza leo, Desemba 24, 2014 baadhi ya walaji wa bidhaa hiyo, wamesema wamezunguka maduka mbalimbali ndani ya mji wa Moshi lakini hawakupata bidhaa hiyo.

Wafanyabiashara wa mji huo wamesema sababu ya kuadimika kwa bidhaa hiyo kunatokana na ongezeko la watumiaji.
 
Mbwembwe nyingi kumbe mnakula mikate kama Wayaudi.
 
Back
Top Bottom