Mike ‘Iron’ Tyson asimulia mikasa, vituko, ukatili katika maisha yake ya ujanani

Mike ‘Iron’ Tyson asimulia mikasa, vituko, ukatili katika maisha yake ya ujanani

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Pamoja ya kuwa mbabe alikuwa anaogopa kwenda jela

Jinsi Mike Tyson alivyojaribu kwenda kwa mchungaji kuhani asifungwe gerezani baada ya kumdhalilisha mpenzi wake katika simulizi hilo jipya Mike ‘Iron’ Tyson anazungumzia maisha yake ya kikatili enzi hizo.

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani (Heavyweight) anasimulia maisha yake ya kufilisika, madawa ya kulevya, ulafi katika maisha na kuvunjika kwa ndoa zake kadhaa tangu enzi za Robin Givens.

Anasema pamoja na yote hayo lakini amejitahidi kuwa baba mzuri na mume safi kwa watoto na mke wake mpya, Tyson amesema kwamba kufungwa jela kumemsaidia kubadilika kwa sababu bila hivyo angekuwa mtu wa ovyo sana na mkatili.

Amesema kwenye mazungumzo na gazeti moja huko nchini Marekani kwamba hakuwahi kupata malezi bora ya mama wala baba kwani mama yake alikuwa mnywaji sana wa pombe na mara nyingi alikuwa analala na wanaume wengi kila siku katika sehemu waliyokuwa wakiishi.

Alifafanua kwamba alikuwa anapenda kutizama mikanda ya cinema ya Mohammed Ali ‘The Greatest’ ambayo ilimsaidia kufikia ndoto zake za kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu duniani na mwanamasumbwi.

Anasema kuwa mke wake wa kwanza Robin Givens na mama yake walikuwa wasanii nguli katika maisha na makahaba lakini pia kama haitoshi mke wake wa pili alimdanganya Tyson kuwa ana ukimwi lakini kumbe ulikuwa uongo mtupu.

Wakati wa Kusikiliza kesi yake ya ubakaji Tyson alikuwa anadhani ni kitu cha kawaida pindi Jaji Patricia Gifford alivyokuwa akisoma hukumu ya ubakaji, ilikuwa ni Machi 26, 1992, wiki sita baada ya kukaa lupango alipokuwa akisomewa hukumu ya kumbaka na kumdhalilisha mrembo Desiree Washington (18) alikuwa anakabiliwa na adhabu ya miaka sitini jela.

Lakini kesi hiyo ilikosa ushahidi wa kutosha kwamba Tyson alimbaka mrembo lakini kosa la kudhalilisha (Sexual harrassement) lilifanya afungwe miaka sita lakini alikaa miaka mitatu jela.

“siku ya hukumu na kutiwa hatiani ya kwenda jela miaka sita nilijua ndio siku ya kuokolewa toka katika maisha ya ovyo, kiburi, ukatili na ulevi wa madawa ya kulevya umewadia,” amesema Tyson

Alizaliwa katika Hospitali ya Cumberland katika Fort Greene, Brooklyn, Tyson kamwe hakuwahi kumjua baba yake mzazi lakini cheti cha kuzaliwa kimeandikwa Percel Tyson mtu ambaye anaamini ndio baba yake mzazi lakini hajawahi kukutana naye.

Mama yake Loma Mae anasema 'baba yake wa kibaiolojia, ni ' Jimmy ' Curlee ' Kirkpatrick Jr.’

Anasimulia zaidi kwamba mama yake alivyopoteza ajira kama matron katika nyumba ya wanawake mahabusu katika jiji la Manhattan ndipo alipoanza kunywa pombe masaa 24 na kulala na wanaume ovyo.
 
Back
Top Bottom