Mike Tyson mzee wa KO aonekana yupo hoi

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827



Mkongwe wa ndondi Mike Tyson (56) ameonekana akiwa mdhoofu kwenye kiti cha magurudumu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Miami Nchini Marekani.

Tyson ambaye ni mmoja wa mabondia waliofanikiwa sana kwenye mchezo huo Duniani alistaafu mwaka 2005, hata hivyo amekuwa akirudi ulingoni mara kadhaa katika mfumo wa maonyesho.

Taarifa zinasema kuwa Tyson anasumbuliwa na matatizo ya mgongo yanayotokana na jeraha.

Hivi karibuni akiwa jijini New York bondia huyo mstaafu alihitaji kutumia fimbo ili kuweza kupata balansi ya kutembea.

Picha hizi zimezua wasiwasi kati ya mashabiki zake baada ya hivi karibuni Tyson kuutabiri mwisho wake kupitia kipindi cha HotBoxin ambapo alisema.

”wote tutakufa siku moja bila shaka. Nikijiangalia kwenye kioo, nayaona mabadiliko usoni mwangu, hii inaamaanisha tarehe ya kumalizika kwangu iko karibu.
 
Hivi yule Tyson wetu wa kijani yuko wapi
 
Mbona picha zinaonesha hajadhoofu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…