20 October 2024
Mikoa yavunja rekodi kujiandikisha uchaguzi wa TAMISEMI 2024
Mikoa mitano ya Tanganyika iliyoongoza nchini Tanzania ni kama ifuatavyo :
Hakutakuwa na siku ya nyongeza ikifika saa 12 jioni itakuwa mwisho wa uandikishwaji, na hakuna siku za nyongeza kuandikisha wapiga kura katika daftari ya wapiga kura wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametoa tathimini ya uandikishaji katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali Mitaa huku akitaja mikoa mitano vinara wa kuandikisha.
Mchengerwa ametoa tathimini hiyo leo Oktoba 20, 2024 akiwa katika Tarafa ya Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mohammed Mchengerwa amefunga zoezi la kujiandikisha kupiga kura na kutoa taarifa ya siku Tisa ya waliojitokeza kujiandikisha nchini ambapo Watanzania zaidi ya milioni 26 wamejiandikisha sawa na asilimia 81.15 ya Watanzania wamejiandikisha.
Mheshimiwa Mchengerwa amejiandikisha katika kituo cha uandikishaji cha Umwe Mchikichini kilichopo Jimboni kwake Ikwiriri Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo alitumia nafasi hiyo kuzungumza na wananchi na waandishi wa habari jimboni kwake mara baada ya kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura na kumesema kuwa zoezi hilo litafungwa ifikapo saa12 jioni leo.
Mhe.Mchengerwa amesema kuwa taarifa ya jumla itatolewa ifikapo saa sita usiku leo muda hautaongezwa.
"Amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mpigakura kote nchini ambapo waliojiandikisha kwa mujibu wa taarifa ya awali ni asilimia hizo 81. 15
"Mtakumbuka kuwa kwa muda wa siku 9 sasa toka tarehe 11 Oktoba, 2024 Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wamekuwa katika zoezi la kuandikisha Watanzania watakaoshiriki zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa itakapofika tarehe 27 Novemba, 2024. Uandikishaji huu unafanyika kwa muda wa siku 10 hadi tarehe 20 Oktoba, 2024" alisema Mchengerwa.
Alisema uandikishaji na maandalizi ya orodha ya wapiga kura wa Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mita ni takwa mojawapo la Kanuni za Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za mwaka 2024.
"Kanuni hizo zinaelekeza kuwa kutakuwa na orodha ya wapiga kura ambayo itatumika katika uchaguzi wa kuwachagua mwenyekiti wa Kijiji, mwenyekiti wa mtaa, mwenyekiti wa kitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa" alisema.
"Nimeona nikutane nanyi ili kuwafahamisha Watanzania kuhusu mwenendo wa uandikishaji huo hadi kufikia siku ya 9 tarehe 19 Oktoba, 2024 na kutoa wito kwa Watanzania ambao hawajajitokeza kujiandikisha watumie siku ya leo ambayo pia ni siku ya mapumziko" alisema.
"Jumla ya wapiga kura 26,769,995 wamejiandikisha kupiga kura sawa na asilimia 81.15 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579 kwa siku zote 10 ambapo wanaume ni 13,033,988 sawa na asilimia 48.69 ya watu wote waliojiandikisha kwa tarehe 11-19 Oktoba, 2024 na wanawake ni 13,736,007 sawa na asilimia 51.31 ya watu wote waliojiandikisha"
"Kwa ujumla, mwenendo huu ni mzuri sana, na kama utaendelea hivi kwa siku ya leo, uwezekano wa kufikia malengo ya uandikishaji ni mkubwa. Hii ni kwa kuwa kuanzia siku ya 5 hadi ya 9 kumekuwa na kuongezeka kwa idadi ya Watanzania waliojitokeza kujiandikisha
Siku ya 5 tarehe 16 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 2,460,664 sawa na asilimia 7.46 ya lengo la siku" alisema.
"Siku ya 6 tarehe 16 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 2,472,605 sawa na asilimia 7.50 ya lengo la siku; siku ya 7 tarehe 17 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 2,971,219 sawa na asilimia 9.01 ya lengo la siku; Siku ya 8 tarehe 18 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 3,409,211 sawa na asilimia 10.33 ya lengo la siku; siku ya 9 tarehe 19 Oktoba 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 3,813,999 sawa na asilimia 115.6 ya lengo la siku
Soma Pia:
Taarifa ya nchi nzima kuhusu mikoa yote iliyotekeleza zoezi la uandikishwaji katika daftari la mpiga kura maalum kwa ajili ya Uchaguzi wa November 2024 itatolewa leo saa Sita Usiku wa manane tarehe 20 October 2024
Mikoa yavunja rekodi kujiandikisha uchaguzi wa TAMISEMI 2024
- Tanga asilimia 101.13 ya lengo ,
- Pwani 98.74% ya lengo ,
- Mwanza 94.09%, ya lengo
- Dar es Salaam 86.66% ya lengo
- na Dodoma 80.63% ya lengo