Mikoa saba kupata mvua kuanzia leo usiku

Mikoa saba kupata mvua kuanzia leo usiku

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia pamoja na Uguja na Pemba yatapata mvua nyepesi kuanzia leo saa 3:00 usiku.

"Angalizo la mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba),"imesema taarifa ya TMA ya saa 24 iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 16, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uwezekano wa kutokea kwa athari ni wastani na shughuli zinazotajwa kuathirika ni za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji wa baharini.

Mbali na maeneo hayo, mikoa ya Kagera na Geita nayo itakuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua wakati mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu na Mwanza itashuhudia hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

"Mikoa ya Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora na Katavi,Morogoro, Manyara, Arusha na Kilimanjaro, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe zitashuhudia mawimgu kiasi na vipindi vya jua," imeeleza taarifa hiyo ya TMA.

Soma Pia: TMA: Kutakuwa na Upepo Mkali unaozidi Kilomita 40 kwa siku 3 mfululizo nchini

Chanzo
: Mwananchi

Haya mliokuwa Majirani huko Kawe akina Mama Kessy, hapo Mtoni kwa Wachimba Mchanga, mnaokaa Makongo jirani na kwa Mzee Juma hadi hapo Bondeni usawa wa Marehemu Komba na kuelekea Daraja la Malecela Mbezi Beach tafadhalini Usiku wa leo kuweni Makini au mkiweza laleni kabisa na Maboya Miilini mwenu ili hata hii Mvua Kubwa ikija na kuwakuta Mmelala ikiwabeba pamoja na Vitanda vyenu muweze Kuelea na Kesho Asubuhi Watu wa Red Cross watakuja Kuwaokoa sawa?
 
Mpaka sasa holaaaaaa. Utabiri wa Hali ya hewa hawa TMA na Sangoma hakuna tofauti wallah.
 

Attachments

  • 20240703_163545.jpg
    20240703_163545.jpg
    43.4 KB · Views: 5
Tunaomba ushuhuda kwa maeneo tajwa huku kwetu hakujatokea kitu
 
Back
Top Bottom