Mikoba ‘inavyowapa ulemavu’ wanawake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532



Wanawake wengi hupenda kubea mikoba kwa ajili ya kubeba vitu atakavyohitaji kutumia muda atakaokuwa nje ya nyumbani au pindi dharula itakapotokea. Imezoeleka kwa wanawake wa rika mbalimbali kuonekana wakiwa wamebeba mikoba jambo ambalo wabunifu wa mitindo huiona kama fursa ya kujitengenezea kipato.

Kumekuwa na utengenezaji wa mikoba mingi ili kuendana na wakati mfano mikoba ya kubeba kwende kumbi za starehe,wakati wa shughuli mbalimbali,maofisini na hata safarini. Mara nyingi katika mikoba ya wanawake utakuta vitu kama simu, lipstick, poda, kioo, kanga na vitu vingine ambavyo anaweza kuhitaji kuvitumia.

Kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake binafsi kuhusiana na ubebaji wa mikoba kwa wanawake kuwa ni jinsi gani unaweza kusababisha madhara au la.

Watu wengi wamezoea kutumia mkono mmoja au bega moja katika ubebaji wa mikoba yao na hata kama ikitokea akibeba mkono ambao haujazoea basi atalirudisha katika mkono ambao siku zote amekuwa akiutumia.

Ubebaji wa mikoba hii kwa muda mrefu unaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa wanawake kama hautadhibitiwa hasa kubeba mabegi hayo kwa muda mrefu tena kwa Staili mbalimbali.

Daktari bingwa wa mifupa na viungo kutoka nchini uingereza Sammy Margo alipokuwa akifanya mazungumzo na kituo cha habari CBS alieleza madhara yanayoweza kumpata mtu anayebeba mkoba katika dizaini tofauti na kushauri nini cha kufanya.

Ubebaji mkoba kwa mbele
Ubebaji wa mkoba kwa mbele chini kidogo ya tumbo kwa kutumia mikono miwili maarufu kama (The twofer clutch). Dk Margo anasema namna hii ya ubebaji inasababisha madhara kwa sababu hufanya mabega kuchongoka kuelekea mbele na pia kuufanya mgongo kutengeneza umbo kama nusu duara.

Pamoja na hayo pia huweza kuifanya misuli iliyo mbele ya mabega kufupika na kukaza huku misuli ya nyuma ya mabega kuwa mirefu na dhaifu.
Hivyo kukosekana kwa uwiano huu husababisha matatizo ya mabega na maumivu ya mgongo.

Ubebaji wa mkoba kwa kutumia sehemu ya juu ya kiwiko
Dk Margo anasema ubebaji huu huweza kuwa na madhara kwa sababu mkoba unapowekwa sehemu ya juu ya kiwiko huifanya misuli ya mkono kufanya kazi ya ziada.

Kama mwanadada hubeba mkoba wake namna hii basi atasababisha kuvutika kwa misuli katika kiwiko na sehemu za misuli mikubwa ya mkono. Uning’inizaji mkoba katika kiganja cha mkono

Dk Margo anasema ubebaji wa mkoba kwa mtindo huu kwa kiasi kikubwa husababisha maumivu ya mgongo, shingo na kufanya mabega kutokuwa na usawa au kupishana(bega moja kuonekana limepanda lingine limeshuka).

Wataalamu nchini
Mtaalamu wa mifupa,misuli na mishipa wa kituo cha Esperance Health care, Christopher Nyoni, anasema mwili umejengwa kwa mpangilio mzuri wa mifupa na misuli unaomfanya mtu awe imara.

Anasema vitu vyote hivyo vinawezekana kukiwa na uwiano sawa wa kazi za misuli.Na endapo misuli itakosa usawa itakaza na mtu kupata maumivu.

Anasema ubebaji wa begi kwa upande mmoja unaweza kusababisha kitu kinachoitwa ‘mascularskeletal injury’ au ‘muscularskeletal disorder’ yaani mjumuiko wa magonjwa yanayotokana na misuli,mifupa pamoja na viungo.

“Madhara haya yanasababishwa mara nyingi na shughuli tunazozifanya, yaani Ergonomics inayomaanisha elimu ya sheria za ufanyaji kazi ambayo inaendana na kifaa unachokitumia kufanya kazi,kazi inayotakiwa kufanyika na uwezo wa mwili wako kufanya ile kazi.

“Hivyo mtu akiwa na uwiano usio sawa wa kazi anayotakiwa kufanya na uwezo wake wa kufanya kazi hiyo, jambo hilo linaweza kusababisha magonjwa ya aina nyingi ya mifupa,” alisema Nyoni

Anasema ubebaji huo huweza kusababisha madhara ya viungo ya aina moja au mbili, hasa ubebaji wa begi kwa upande hadi bega lingine likanyanyuka juu inakuwa ni ishara kuwa tayari umetoka katika utaratibu wa kawaida ya mwili wako.

Anasema ubebaji huu hauwezi kusababisha madhara ya papo kwa papo bali yanakuja kwa muda mrefu na kusababisha misuli ya upande mmoja kukaza na baadae huweza kusababisha matatizo ya shingo, bega na mgongo.

Nini kifanyike
Anasema kitu anachotakiwa kukifanya mtu anayependa kubeba begi, ni kuepuka ubebaji wa mizigo mizito iliyozidi kipimo unaoweza kumuondoa katika utaratibu wa mwili wa kawaida.

“Ukibeba begi ukaona bega moja limenyanyuka juu au hadi ukajiona umepinda basi usibebe na kama ni lazima kulibeba basi unatakiwa kubadilisha mikono kila mara, au ukiona bega limechoka weka mkononi,ukona mkono umechoka rudisha begani lakini usiweke katika eneo moja kwa muda mrefu,” anasema Nyoni.

Dk Margo alishauri kuwa njia ya kuepuka matatizo haya ni kubadilisha mkono kila mara pindi unapokuwa umebeba mkoba.



Chanzo: mwananchi
 
Sijui hua wanaweka nini unakuta mtu kabeba mikoba miwili yote imeshibaaa, mpk unamuonea huruma akitembea, lol
 
Ukiona mkoba wa mwalimu utamuonea huruma kwa kweli

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kuna Mama lecturer UDSM ana bebaga mikoba mitatu. Sasa sijui itakuwaje.... Na yote mizito balaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…