Mikogo ya Hemed Kivuyo wa ITV!

Mikogo ya Hemed Kivuyo wa ITV!

Mu7

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2013
Posts
1,624
Reaction score
1,934
Ukweli mie nakereka na mikogo ya huyu mtangazaji anapoanza kuripoti habari za michezo. Anaweza kulembalemba almost dak 2 kabla hajataja tukio lenyewe. Sina shaka na uwezo wake wa kazi ya kuripoti ila mikogo imezidi mpaka anaboa!
 
Anapotaja neno Awali,bado ana ladha ya pekee yake mwacheni atie kogo katika kazi,wewe kwenye kazi yako vipi huweki kogo??

Msubiri kesho saa mbili usiku atavouelezea mchezo wa nani mtani jembe labda akae massari

Bravo Hemed
 
mikogo ikizidi inaharibu
mfano mi cku za nyuma nilikuwa nampenda sana maestro lkn sasa hv nae kazidi mbwebwe mpaka sasa inaonekana ni maringo au nyodo
 
unamjua yule jamaa wa kenya mwendesha kipind cha JICHO PEVU? basi ungemskiliza huyo kivuyo cha mtoto
 
acha wivu wa kike wewe, hakuna mtu aliyekulazimisha kumwangalia
 
Ukweli mie nakereka na mikogo ya huyu mtangazaji anapoanza kuripoti habari za michezo. Anaweza kulembalemba almost dak 2 kabla hajataja tukio lenyewe. Sina shaka na uwezo wake wa kazi ya kuripoti ila mikogo imezidi mpaka anaboa!
Hizo nakshi zake ambazo nyingine zina ladha ya ki-amu[kiswahili] na misemo ambayo imesahaulika ndiyo zinazotufanya wengine tufungue radio one/ITV
 
Ukweli mie nakereka na mikogo ya huyu mtangazaji anapoanza kuripoti habari za michezo. Anaweza kulembalemba almost dak 2 kabla hajataja tukio lenyewe. Sina shaka na uwezo wake wa kazi ya kuripoti ila mikogo imezidi mpaka anaboa!
Angalia tv nyingine na utuache tunaopenda tuendelee kufurahia mbwembwe za kivuyo
 
Awe mbunifu, sio lazima aongee yale yale kila siku. Lazima utamsikia: "Timu hiyo kutoka mtaa wa yule mnyama mrefu na mpole..." au "Timu hiyo kutoka mtaa wenye pilikapilika jijini..."
 
Bora uwe na sura kama kinyago utapendwa na watalii,kuliko huo unafiki ,uzandiki na chuki binafsi zako ambazo utapendwa na wachawi. Tuachie mtangazaji wetu bora zaidi anayejua kukitumia kiswahili fasaha. Kawasikilze kibonde,bibi twelve na madam mchovu
 
Anamuiga George Maratu wa itvvvvvvvv!

Ni afadhari na Kivuyo huyu George Maratu ndo mtangazaji anayeniudhi kuliko wote nadhani kwa namna anavyovuta sauti yake hadi anaharibu I wish asiongezewe mkataba.
 
Back
Top Bottom