Benki na taasisi nyingi za fedha huangalia mambo 5 kama base/kigezo cha kupata mkopo kwao, mambo haya wengine wanayaita 5Cs - yaani:
1. character (integrity) - Tabia yako mkopaji hasa uaminifu, hapa ndio mambo barua za mtendaji wa
kata,kijiji, mtaa, balozi, baba/mama mwenye nyumba, etc
2. capacity (sufficient cash flow to service the obligation)- mzunguko wa fedha wa biashara
yako,kwa siku,wiki,mwezi,mwaka unauza na kutumia kiasi gani? Naamini hapa ndio
walitaka taarifa zako - waone mzunguko wako wa fedha unakuwa mzuri.
3. capital (net worth)- mtaji wako wa biashara, hiki ni kiasi kamili ambacho biashara inamiliki na
hakuna deni (kiasi unachodaiwa), kama ni duka inaweza kuwa mali za dukani,fedha taslimu, au mali
zisizohamishika ila sehamu ya biashara yako - kwamba kama zitaondolewa katika mzunguko wa biashara
basi biashara itayumba, kama ni biashara ya stationary - photocopy mashine,etc
4. collateral (assets to secure the debt)- mali zisizohamishika, hizi zinaweza kuwa zinamilikiwa
na biashara au ni zako unamiliki wewe.
5. conditions (of the borrower and the overall economy)- hii ni hali ya biashara yako na hali ya
uchumi unaozunguka biashara yako, vinalinganishwa na kiasi cha fedha unachotaka kukopa.
kwa hio ndg, benki na taasisi za fedha zinatumia vigezo hivyo kuweza kukukopesha au kukataa, kwa kesi yako - inawezekana kabisa kuwa:
1. hauweki fedha benki, ila kama inaweka basi si mara kwa mara, au ndio umefungua akaunti na kuomba
mkopo.
2. inawezekana biashara yako ina matumizi mengi
3. Vyanzo vya mapato vya biashara yako havijatengamaa, yaani hauna mauzo mazuri
nadhani kwa sasa vigezo hivi vinatosha wengine nao wataongezea, ila kumbuka siku zote benki zinaangalia usalama wa fedha zao