SoC04 Mikopo kwa wahitimu wa vyuo vikuu ni suluhisho la ajira kwa vijana, na mwanzo Bora kwa Tanzania tuitakayo

SoC04 Mikopo kwa wahitimu wa vyuo vikuu ni suluhisho la ajira kwa vijana, na mwanzo Bora kwa Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Fad_Jr

New Member
Joined
May 27, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Utangulizi: Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikiwekeza sana na kimkakati zaidi katika sekta ya Elimu.

Sekta ya Elimu ndio sekta muhimu kuliko sekta zote hasa ukifikiria kuwa ndio sekta inayondaa watumishi wa sekta zingine.

Ufanisi na weredi wa wafanyakazi ndani ya sekta yoyote unategemea elimu,ujuzi,maarifa na nidhamu waloipata katika sekta hi ya elimu.

Sambamba na serikali ya JMT kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wenye sifa maalumu Kama zinavyo ainishwa ni Bodi ya mikopo ya vyuo vikuu(HESLB) Lakini changamoto imekuwa kubwa na mbaya kwa ukubwa zaidi hasa vijana hawa vyuo vikuu wanapo hitimu masomo yao.kwani wengi wa wahitimu Hawa hurudi majumbani kwao wakiwa na elimu au ajuzi Ila wanakosa uzoefu ambacho ndio kigezo kinacho watesa wahitimu hao katika kuajiliwa katika sekta za uma na sekta binafsi.hivyo kubakia bila kuzalisha chochote kinacho Saidia taifa na kuchelewa zaidi kulipa mikopo yao.hivyo kubakia majumbani kwao,mijini,vijijij na mitaani,wengine kuwa wezi,wazinzi,matapeli na kufanya matendo maovu ambayo kwayo wanahisi ni vyanzo vya pesa bila kujali na kutathimi hatari ya shughuli hizo juu ya afya zao,familia zao na taifa kwa ujumla.

Maoni yangu:
Serikali iwape mikopo maalumu wahitimu wa vyuo vikuu nchini.
Kama ambavyo ilivyokuwa ikiwapa mikopo walipokuwa vyuoni.
Napendekeza utaratibu wa mikopo hu uwe Kama ifuatavyo;
_Wale walokuwa wanapata mikopo wakiwa chuoni basi wapewe mikopo hu pindi tu matokeo yao yanatoka na ikiwa ameafaru.
_Muhitimu kabla ya kumaliza aandiki proposal ya biashara ambayo angependa kufanya au kujiajiri Kama mjasiriamali.
_Iundwe Bodi maalumu ya kusimamia mikopo hi ambayo itakuwa na angalau mjumbe mmoja katika kila chuo kikuu nchini,ambae mjumbe huyu atakuwa ni mkufunzi wa chuo husika.
Faida ya mikopo hi pamoja na
Kuwapa fursa ya kujiajiri kwani watakuwa na mtaji,kupunguza vitendo viovu mjini na vijijini,kuongeza Pato la taifa,kuanzia kurudisha mikopo ya Heslb kwa wakati,kuwapa uwezo wahitimu kuanza familia Bora ambayo ndio chombo Cha maadili katika jamii.
Tanzania tuitakayo itawezekana tukiwawezesha vijana waleo,hasa wahitimu wa vyuo vikuu nchini.

Naomba kuwasilisha
asanteni.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom