Mikopo mtandaoni bado ni Changamoto kubwa ya kuaibisha wakopaji kwa ndugu, Jamaa na marafiki

Mikopo mtandaoni bado ni Changamoto kubwa ya kuaibisha wakopaji kwa ndugu, Jamaa na marafiki

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Baadhi ya App za Mikopo zinatesa wananchi wanaandika wanakopesha kwa siku 100 lakini baada ya siku nane wanadai wananchi.

Riba zao pia ni kubwa sana na ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida.Serikali ifuatilie hili kwa kina kama haina maslahi nalo.

Wananchi pia wapewe uelewa kuhusu Mikopo hii.

Lakini pia kuna haja gani ya kumtumia mwananchi meseji zaidi ya 50 kumdai na kumpigia pigia simu na maneno ya matusi.

Kumuaibisha mtu kutamfanya aweze kujizulu.

Tabia hii ni mbaya na waache maramoja.

Wananchi tupaze sauti kwa Nguvu serikali ilifanyie kazi maramoja.
 
Mkopo mtandaoni ni Kama kutafuta mchumba mtandaoni....! huwezi pata mchumba wa Maana...! Utapata gube gube likutese
 
Back
Top Bottom