Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kwenye vyombo vya habari madhila wayapatayo wakopaji wa taasisi za mikopo midogomidogo hususani akina Mama inaonekana sauti ya vilio ni kama imepanda zaidi.
Kwanza kabisa taasisi hizo pamoja na kupewa jina baya kana kwamba zinakosea sana ni zao la mifumo mibovu iliyojaa urasimu mwingi ya kibenki. Watanzania walifurahia sana kipindi cha uanzishwaji wa benki ya "National Microfinance Bank" iliyobeba jina la makabwela ila kiuhalisia makabwela hawaaminiki hata kidogo.
Maadili mabovu yaliyotukuza yametuaondolea Watanzania wengi uaminifu na kuaminika siyo tu na taasisi za kifedha ila hata vyombo vya Serikali vinapotaka kuisaidia jamii kiuchumi hujikuta katika pata potea.
Elimu ya fedha "financial education" ni janga la Taifa linalosubiri kutangazwa tu. Ni suala la muda tu uhalisia hauvumilii kufichwa. Elimu tunayofundishwa inatuandaa kujiajiri au kuajiriwa na imeacha ombwe kubwa la Usimamizi wa fedha inayotokana na ujira ndiyo maana leo mfanyakazi anapewa elimu ya matumizi ya pesa anapofikia umri wa kustaafu Ili asichanganyikiwe zaidi.