A
Anonymous
Guest
Rasmi dirisha la usajili wa vikundi pamoja na maombi ya mkopo ya halmashauri ile ya 10% (vijana, wanawake na walemavu) vilifunguliwa mwezi wa 10, 2024.
Awali iliionekana kuwa tutahudumiwa vizuri na kwa wakati. Lakini mpaka sasa bado hatujahudumiwa mikopo hiyo zaidi tu ya kupigwa picha mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh 400 millions kwa vikundi (37) vilivyokidhi vigezo baada ya kukaguliwa na kuidhinishwa.
Tuliambiwa kuwa ndani ya wiki moja toka tarehe 29/1/2025 tutakuwa tumeingiziwa hela lakini hadi sasa bado hakuna chochote na wala hatujui hatma ni ipi hadi leo hii.
Wakati Mama anafanya jitihada za kukwamua wimbi la ajira kwa kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu ili wajiajiri, bahati mbaya ni kuwa jitihada hizi zinakwamishwa na watendakazi wake wanaoendekeza uzembe kwa kutothamini nafasi walizokabidhiwa huku sababu zikiwa ni zile zile kila siku kuwa mkurugenzi hajasaini bado.
JF, tusaidieni kupaza sauti zetu, Nzega iangaliwe.