Mikopo ya Benki

Mikopo ya Benki

Sim Card

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2019
Posts
881
Reaction score
1,601
Wadau mimi mzima najihami na janga hili la COVID 19. Natumaini tuko pamoja pia.Mimi ni mwajiriwa katika sekta binafsi.Jana Ijumaa,mwajiri wangu alitoa barua kwa wafanyakazi wake kuwa kuanzia mwezi huu wa May mwishoni atalipa mishahara nusu na kuanza kutoa likizo bila malipo endapo janga hili litaendelea baada ya hapo.

Yaani June na kuendelea. Nina mkopo benki ambao nategemea kumaliza Disemba 2020.je wadau, benki iliyonikopesha inaweza kunifanyia marekebisho ya mkopo nilipe kiasi ili nisiende bila chochote nyumbani endapo nikiongea nao? Natumaini janga hili litapita tutakuwa salama tena. Naomba ushauri wenu.Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua sio kwamba benki ndo huwa wanakata fedha laaaah hasha, ila muajiri wako ndio huwa anawapelekea pesa, so ni issue ya kuyajenga na Mwajiri wako, thou mkopo unaweza kwenda muda mrefu na hivyo makato yakaongezeka kwa muda mrefu baada ya halivya uchumi kutengamaa

Au mnasemaje mods wa JF
 
Mkuu kwanza pole kwa hilo janga ingawa limetukumba wengi.
Ushauri wangu fanya hivi,tafuta wafanyakazi wenzako ambao wana tatizo kama lako kisha muandike barua kwenda kwa mwajiri wenu,then mwajiri wenu ataenda kuongea na watu wa benki kupunguza asilimia za makato au kusitisha makato kadhaa.

Hiyo benki kama ina mahusiano mazuri na kampuni yenu hawatakataa kusikiliza.
Nimeona kampuni fulani wamefanya hizi hatua nilizozisema hapa na wamefanikiwa kupunguziwa makato ya benki maana hali ilikuwa mbaya.
Wadau mimi mzima najihami na janga hili la COVID 19. Natumaini tuko pamoja pia.Mimi ni mwajiriwa katika sekta binafsi.Jana Ijumaa,mwajiri wangu alitoa barua kwa wafanyakazi wake kuwa kuanzia mwezi huu wa May mwishoni atalipa mishahara nusu na kuanza kutoa likizo bila malipo endapo janga hili litaendelea baada ya hapo.Yaani June na kuendelea.

Nina mkopo benki ambao nategemea kumaliza Disemba 2020.je wadau, benki iliyonikopesha inaweza kunifanyia marekebisho ya mkopo nilipe kiasi ili nisiende bila chochote nyumbani endapo nikiongea nao? Natumaini janga hili litapita tutakuwa salama tena. Naomba ushauri wenu.Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri alioutoa mbu wa dengue ndio una uzito kwa sasa, hapo inategemea utaratibu wa makato wa marejesho ukoje. Kuna wale mshahara wote unaenda bank kisha bank wanachukua rejesho lao na wengine mwajiri anakata na kupeleka malipo ya marejesho bank.

Kwa kuongezea tu, serikali kupitia benki kuu wanatakiwa kuingilia kati hili jambo watoe muongozo kwa mabenki kuhusu unafuu wa marejesho ya mikopo hasa hichi kipindi cha Corona.
 
Asanteni japo nimewaza kuwaona physically mimi kama mimi nikiwa na documents zote ili nimsikilize Branch Manager atanushauri vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom