Mikopo ya dharura

Tujikomboe Finance

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
212
Reaction score
81
Kama unahitaji mkopo wa dharura tuwasiliane. Muda wa mkopo ni mwezi mmoja tu. Riba kwa mwezi ni kati ya 20%- 30% kiasi kamili cha riba kinajadilika kulingana na ubora wa dhamana. Dhamana ya mkopo inayokubalika ni gari, na mkopaji awe tayari kukabidhi gari hilo pamoja na nyaraka zake kwa muda wote huo wa mkopo. Hakuna gharama zingine zozote. Ofisi zipo Wilaya ya Temeke Mbagala rangi Tatu. Huduma hii ni kwa ajili ya wateja wote waliopo mkoa wa DSM na Pwani. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba hii 0786 66 30 65 kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi 11.00 jioni Jumatatu- Ijumaa

Karibu
 

Mkopaji akubali kuacha gari au kiwanja,how? Ofisi zenu zipo wapi? Mmesajiliwa? All in all thread yako haijitoshelezi,
 

Shylock at work; Customer be aware!!
 
Mkopaji akubali kuacha gari au kiwanja,how? Ofisi zenu zipo wapi? Mmesajiliwa? All in all thread yako haijitoshelezi,

Maswali yake ndio yamenifanya nijue yeye sio mlengwa.....Sio kila mtu aweza kuwa mteja wako vizuri kulijua hilo.
 
Maximum ya amount na mawasiliano yako tafadhali
 
Post dhaifu kabisa.
1. Hujaeleza wewe ni nani kama taasisi au kampuni
2. Bado unataka watu wawasiliane na wewe bila kuacha namna ya kuwasiliana nawe.
 
Halafu umkute ameukabia Suti yake huyo wakati anaimbisha watu,unaweza kusema Bonge la msomi.
Lakini kujieleza tu tatizo.Wengine tukishindwa maisha tukalime jamani.Mjini joto
 
Halafu umkute ameukabia Suti yake huyo wakati anaimbisha watu,unaweza kusema Bonge la msomi.
Lakini kujieleza tu tatizo.Wengine tukishindwa maisha tukalime jamani.Mjini joto

Mkuu kuna vijana flani wapo Temeke ni jamii ya huyu daa yani ni km utapeli huwa nawaonea sana watu huruma hiyo gari na hati ya shamba wanayokwambia ni kwamba mnaingia nao mikataba wanakupa pesa usipolipa baada ya mwezi mmoja ulichoweka kinakuwa chao haijalishi pesa uliyokopa yani hawa ni zaidi ya wezi
 
Majizi,eti gari na documents zote,,teh teh
 
Kazi nyingine Laana tu kwa mungu,maisha mafupi sana tofauti na tunavyofikiria.
Mungu anaona dhamira zao.
Naamini watatafuta kazi nyingine zakufanya,Banks nyingi sana ndogondogo sasa hivi wanatoa pesa kwa masharti nafuu.
Nimeona wengi sana wenye kufanya hivyo wameacha baada ya kuona hakuna wanalopata zaidi ya laana tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…