MIKOPO YA ELIMU YA JUU; Ombi kwa Mh.Rais kutokana na kauli yake

Handsome Boy 2014

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
605
Reaction score
151
Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa umefika wakati wa elimu ya sekondari kutolewa bure na Wanafunzi wa elimu ya juu walioomba mkopo kupewa wote.Nimuombe Mheshimiwa Rais hebu kauli yake aisimamie kwa vitendo ili watoto wa Watanzania waweze kupewa mkopo ili kumudu kusoma elimu ya juu.
 
ulizia alvyowageuka UKAWA walpokuwa wamekbaliana kuwa mchakato wa katba utaahirshwa mpaka 2016
 
Utegemee kikwete atimize ahadi yake? Umesahau aliposema hahitaji katiba mpya? Umesahau alivowabeza wapinzani walipokuja na mpango wa kuwasomesha bule wanafunzi? Labda umwambie anaitwa marekani hapo anaweza hata asile ili asichelewe. 2015 hawapati kura yangu hata nusu
 
Nimejaribu kufatilia uongozi wa marais dunian kote,bt cjawahi ona rais km wa Tz
 
Hivi kumbe bado wapo baadhi ya Watanzania wanaendelea kumsikiliza Kikwete!!!

Jamani, kama makosa kweli tuliyafanya mwaka 2005. Binafsi nilimdharau huyo Kikwete tangu 2008 (kwenye suala la Rich Mond), pia suala la EPA pamoja na madawa ya kulevya.

Hapa nilipo simtambui Kikwete kama ni rais na maisha yangu yanaendelea kama kawaida (namshukuru The Almight).

Hivyo, jitahidini kutazama njia zingine mbadala ili muweze kuishi maisha yenu, ila msiitegemee serikali ya huyo Kikwete.
 
duuh...kweli hii ni dalili ya wananchi kukata tamaa na Viongozi wao waliopo madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…