Mikopo ya "Kausha Damu": Suluhisho la muda mfupi lenye madhara ya muda mrefu

Joined
Aug 18, 2022
Posts
7
Reaction score
16
Mkopo wa Sh. 100,000 — Hesabu Halisi
Pasaka hii nilikuwa napiga story na baba mdogo wangu huku kigamboni kuhusu mikopo “kausha damu”. Alipata mkopo wa Sh. 100,000 kwa muda wa siku 30, na malipo ya Sh. 4,000 kwa siku. Kwa njia hiyo, malipo ya jumla yanafika Sh. 120,000
Ukiangalia kwa haraka haraka, mkopo huo una riba ya "asilimia 20 kwa mwezi." Mtu anaweza kujisemea kwamba akipata huo mkopo, ana uwezo wa kupata pesa zaidi ya sh.120,000 ndani ya mwezi mmoja. Lakini hapa ndipo tatizo linapoanza. Kiwango hicho cha 20% ni nominal interest rate tu, si gharama halisi ya mkopo.
Kwenye ulimwengu wa fedha, kujua kwamba mkopo huu ni mzuri au mbaya, huwa hatuangalii nominal interest rate (riba unayoambiwa pindi unapoomba mkopo) ila tunaangalia Effective Interest Rate
Effective Interest Rate ni riba halisi unayolipa kwa mwaka kwa kuzingatia mkopo uliopata, marejesho unayolipa pamoja na muda wa huo mkopo bila kujali jinsi riba inavyotangazwa na mkopeshaji.
Mkopo huu una effective interest rate ya 1.219% kwa siku ambayo ni sawa na 43.8% kwa mwezi (kwa sababu unafanya marejesho kila siku) na sio “20%” ulioambiwa hapo mwanzo. Sasa kwa kujua hilo, fikiria hivi: biashara nyingi za kawaida hapa Tanzania, maduka ya rejareja, mama lishe, bodaboda, zina return on capital employed (ROCE) (faida ÷ mtaji uliotumika) ya kati ya 12–18% kwa mwaka. Nakumbuka sisi tulikuwa tuna duka la rejareja, ingawa tulikuwa tunapata sh. 200,000–500,000 kwa wiki, ROCE yetu kwa mwaka ilikuwa kati ya 12–18%. Ukiwa na mkopo wenye effective interest rate ya 43.8% kwa mwezi, gharama ya mkopo inazidi mapato ya mtaji wako kwa mbali. Biashara inaweza bado kufanya faida ya jumla, lakini kila siku ya malipo ya sh. 4,000 inafuta mtaji wa kufanyia kazi ambao ungehitajika kununulia bidhaa, na hapo ndipo mzunguko mbaya unapoanza.
Sasa kwa mkopo wenye “riba” ya 20% kwa mwezi, utalipa jumla sh. 120,000 mwisho wa mwezi. Ila kwa vile mkopo wenyewe ni “kausha damu”, unashangaa hadi mwisho wa mwezi mkopo huo hujaleta tija yeyote kwenye biashara yako, na unalazimika kukopa tena. Fumba fumbua, mwaka mzima umeisha kwenye hii mikopo kwa sababu tatizo la msingi la cashflow halikuwahi kutatuliwa.

Tatizo la Kimsingi: Mzunguko Mbaya wa Fedha
Mikopo hii haifanyi biashara kuwa hasara mara moja, faida ya jumla inaweza bado kuzidi hiyo riba. Lakini hapa ndipo mtego wa kweli unapoanza: malipo ya Sh. 4,000 kwa siku yanafuta mtaji wa kufanyia kazi (working capital) ambao ungehitajika kununulia bidhaa za kutosha. Biashara inauza kidogo kwa sababu ina stock ndogo, na faida ya jumla inashuka. Wakati huo huo, tatizo la asili la mtiririko wa fedha (cashflow) bado halijatatuliwa. Mwezi unaofuata, pengo lile lile linarudi. Mkopo mwingine unachukuliwa. Kila mzunguko unaweza kuonekana unaomuacha mkopaji hai, lakini kila mzunguko unamomonyoa akiba, unampunguzia uwezo wa kufanya biashara, na kumfanya ategemee mkopo zaidi kuliko awali.
Tafiti mbalimbali za microfinance, ikiwemo ripoti ya Consultative Group to Assist the Poor (CGAP) ya mwaka 2022 zinaonyesha kwamba kaya zinazopata mikopo hii ya kausha damu huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupoteza mali zao, biashara, vifaa ndani ya miaka miwili kuliko zile zinazokopa benki za kawaida.
Mfano, tulinganishe wakopaji wa aina mbili, anayekopa kila mwezi kwa hawa mikopo kausha damu na anayekopa benki ya kawaida

Kwa hiyo, badala ya kuingia kwenye mikopo kausha damu kila mwezi, ni heri mtu aende kuomba mkopo benki wa mwaka mmoja ingawa kwa wengi wetu, hilo si chaguo linalopatikana kwa urahisi. Benki zinahitaji dhamana (collateral), rekodi za miamala, leseni ya biashara, na historia ya akaunti ya miezi sita au zaidi. Mkopaji wa mikopo kausha damu mara nyingi hakosi haya yote. Ndio maana mikopo hii inastawi, inajaza pengo ambalo benki hazijawahi kulifunika.

Hatua za Kubadilisha Mfumo, Si Kulaumu Watu
Tatizo hili si la watu maskini kukosa akili za fedha. Ni tatizo la kimfumo: watu hawa wanakosa ufikiaji wa mfumo rasmi wa benki kwa sababu hawana rekodi za miamala ya benki, hawana dhamana, na mapato yao ni ya kila siku si ya kila mwezi. Suluhisho lazima lizingatie ukweli huu.

1. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Iweke Ukomo wa riba halisi (Effective interest)
Hii ndiyo hatua ya kwanza na yenye nguvu zaidi. BoT ina mamlaka ya kisheria ya kuweka ukomo wa riba halisi kwa taasisi zote za fedha ndogo, si riba ya kawaida inayoweza kupotoshwa kwa maneno mazuri, bali effective interest yenye uwazi kamili. Afrika Kusini, kupitia National Credit Act (NCA), ni mfano bora wa jinsi hii inavyoweza kufanyika: NCA inaweka ukomo wa riba kulingana na aina ya mkopo na inaunganisha ukomo huo na kiwango cha riba cha Benki Kuu (repo rate), na hivyo ukomo unabadilika kadri hali ya uchumi inavyobadilika. Zaidi ya hayo, NCA ina kanuni ya “in duplum” — riba, ada, na malipo mengine hayawezi kuzidi jumla ya mtaji wa awali. Tanzania bado haijafanya hivyo kwa kiwango kinachotosha.

2. Kuweka Miundombinu ya Rekodi za Miamala ya Fedha Taslimu
Tatizo moja kuu ni kwamba wafanyabiashara wadogo hawana historia ya miamala wanayofanya. Suluhisho: kampuni za simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money) tayari zina data ya miamala ya miaka mingi. BoT na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaweza kushirikiana kuunda mfumo wa Credit Scoring unaotumia data hii, kinachojulikana kama "alternative credit scoring." Kenya ya M-Shwari, ingawa si kamili, inaonyesha mfano huu unaweza kufanya kazi.

3. SACCOS na Vikundi vya Kuweka na Kukopa (VICOBA)
SACCOS na VICOBA ni mifano ya asili ya Tanzania ambayo tayari inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Lakini mifano mingi bado inakosa mtaji wa kutosha na mafunzo ya usimamizi. Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inaweza kuongeza msaada wa kiufundi na mtaji mdogo wa awali (seed capital) kwa vikundi hivi badala ya kutegemea MFI za nje.
.
 
Umefafanua vizuri ila wengi hawana elimu kwenye hili, na wengi hawana uwezo wa kwenda bank. Hii mikopo umiza imesoma mapungufu yaliyopo kati ya mwananchi wa kawaida asiye na vigezo vinavyohitajika bank, akaamua kuja na mfumo unaoonekana ni mrahisi Ila Una gharama kubwa.
Ukisema warejeshe mwisho wa mwezi inaweza ikawa changamoto kwao, angalia zile App za mikopo, baadhi zina utaratibu mzuri wa marejesho mwisho wa mwezi, ila wengi hawarejeshi kwa wakati na wengine kuvunja laini.
 
uko sahihi gentleman,
kausha damu imewatesa na kuwafedhehesha sana akina lema na heche aise, mpaka leo bado inawakamua yaani
 
shida zote hzi tunajiletea sie wenye kwa kutokuwa waaminifu. watu wangekuwa wanakopeshana tuu vizuri ila ndio hivyo ukiwakopesha wanapotea mazima wacha wakakope kwenye kausha damu na kwenye chupi mkononi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…