Mikopo ya nyumba


You are right mkuu, ikiwa mtu unalipa kodi ya nyumba kati ya 80,000 - 100,000 -150,000 mpaka 200,000 ni bora ukacheck uwezekano wa kukopa. Maana ukipanga consecutively miaka kumi. Itakuwa heri aliyekopa maana ataendup kuwa na nyumba.
"Change Favours The Prepared Mind"
 

kwanza inabidi uondokane na swala la ubinafsi, badala ya kujifikiria wewe tu inabidi ufikirie familia

kama wewe ni mwalimu na mshahara wako ni laki na nusu, nitakushauri umwambie mme/mke wako ili mchanganye kipato chenu na nyumba iwe yenu wote.
mfano ukichanganya kipato chako na cha mme wako ambacho ni 650,000 jumla inakuwa 800,000.
kwa hiyo 30% ya 800,000 kila mwezi ni 270,000 kwa miaka 15 ni 48,600,000.
kwa maana hiyo unaweza ukapata mkopo wa mil 28 na mil20 ikawa interest ya benki.

na kama wewe ni single parent ningependa kukutaarifu kuwa mortage hata ulaya sio kila mtu anaweza kuafford.
wazungu wanakitu kinaitwa property ladder, yani unaanza kununua nyumba ya chumba kimoja au viwili alafu baadae unaiuza na kununua nyumba kubwa zaidi kutokana na kukua kwa familia yako/mahitaji sambamba na kipato
 

unauwekea bima mkopo unaochukua, kwa hiyo ukipunguzwa bima inaendelea kulipa.
nina rafiki muindi alikata bima ya mkopo wa nyumba ambayo ilikuwa inamlinda kama akifukuzwa kazi sio kwa kosa lake mwenyewe na pia crtitcal illness. kwa bahati mbaya mke wake akapata cancer ambayo inakuwa classfied as critical illness. Bima ikalipa mkopo wote uliobakia pamoja na hela juu.
 

...safi sana kwa uchambuzi yakinifu.
Wazo la property ladder ni zuri sana. Unaangalia uwezo wa mfuko wako, kisha unachagua eneo ambako mfuko wako + Mkopo huo wa Bank utakuwezesha kununua nyumba kwa gharama nafuu sana.

Pia, waweza nunua nyumba kuu kuu na kuifanyia ukarabati, kisha kuiuza. Pesa ipatikanayo utanunulia nyumba yenye thamani zaidi, na mzunguko unaendelea hivyo hivyo mpaka kufikia malengo yako.

It's all about patience and commitment. Kila kitu kinawezekana, nia tu.
 
binafsi naona azania bank ndio wazuri kwa mambo ya mortage TZ. wao wanaruhusu kama una kiwanja wanakupa mkopo wa kujenga nyumba. hii ni nzuri sana kwa ajili nyumba ambazo zimemalizika bei yake iko juu sana.

angalia housing construction kwenye hiyo link hapo chini

link hii hapa http://www.azaniabank.co.tz/azania/homeloan.htm
 
mkuu inategemea na maeneo ila hiyo pesa unajenga nyumba safi kabisa ya adabu

mkuu taratibu bwana, nyumba safi na ya adabu kwa milioni kumi na tano, hiyo nyumba ni ya chumba kimoja au?
 
mkuu taratibu bwana, nyumba safi na ya adabu kwa milioni kumi na tano, hiyo nyumba ni ya chumba kimoja au?

cjui unamaanisha nn mkuu banana kipunguni b uwezi amini kwa kududuliza mchanga upo free unapiga tofali zako unaanza kujenga mafundi wapo wa viwango tofauti na gharama tofauti tafuta wa kiwango chako 20 millioni si haba unless unataka ushabiki vinginevyo ni pm kwa ushuhuda live
 
Kama kweli wanaweza kufanya hivyo basi mortage bei zao na security lazima iwe kubwa sana na pia kama tu mikopo ya kilimo ni matatizo je ya nyumba itakuaje??
 
...si mbaya 'wazawa' kufanya investments za BUY-TO-LET (kama hizi) zije zitufae kwenye fainali za uzeeni. πŸ™‚

Hiyo USD 110, 000 ni gharama ya apartment siyo hilo ghorofa mkuu!
 
Hiyo USD 110, 000 ni gharama ya apartment siyo hilo ghorofa mkuu!

...naaaam, nafahamu sana hilo.
Hizo 2# bedroom apartments ndio bei zake hapo Upanga.
Au wewe ulinielewaje?

Kama uwezo unatosha, unanunua apartment kwenye hilo ghorofa na kuikodisha... πŸ™‚
 
mkuu inategemea na maeneo ila hiyo pesa unajenga nyumba safi kabisa ya adabu

Ni kweli kabisa, kuna nyumba ambazo hujengwa kwa ajili aidha kupangisha au kuuza tena basi, mara nyingi sio lazima liwe mansion kuuubwa utapata hasara bure.
Two rooms is an ideal house for most medium income and young couples, jenga vyumba vinne au vitano utauza au kupangisha kwa bei ya hasara, maana wanaozihitaji wachache sana.
 
Kwa taarifa yenu msiojua, moja ya sharti la kupata mkopo wa nyumba stanbic ni kipato cha si chini ya Sh. million 3.5 kwa mwezi .
 
Kwa taarifa yenu msiojua, moja ya sharti la kupata mkopo wa nyumba stanbic ni kipato cha si chini ya Sh. million 3.5 kwa mwezi .

...dah, very discouraging news.
Anyway, wakisema kipato haina maana mshahara pekee.

Huenda mtu ukawa na steady income ambayo inaweza ikawa inakuingizia hizo 3.5m tshs kwa mwezi vile vile, i.e biashara, na hata kama unawapangaji vile vile ambao hukuwezesha kufikisha hiyo amount kila mwezi. Au?
 
...si mbaya 'wazawa' kufanya investments za BUY-TO-LET (kama hizi) zije zitufae kwenye fainali za uzeeni. πŸ™‚

Mazee hii Upanga sehemu gani? Watu hatutaki kukesha kwenye foleni wakati tunarudi Tegeta au Kibaha.

Jamaa wana sq metres/ feet? Plans? Picha zaidi? Wanaweza kuchukua 10% down? Wanatoa mortgage kwa vigezo gani maana ninavyojua bongo hamna credit report/ bureau so far.

Mtu unaweza kuwaachia 10-30% ukawaweka wadogo while unaangalia ustaarabu mwingine, najua kuna watu wanaona viota hatari lakini kama sq footage zinahusika na plan imeenda shule haiko mkinga.
 

...hilo la kuepuka foleni neno juu ya mstari.
Apartments blocks hizi zinajengwa kwa 'fujo' mitaa ya Upanga mashariki na Upanga magharibi.

Ukiwa una drive United Nations road lazima utayaona tu maghorofa haya 'yakikwangua anga!'.
Ukiingia mitaani Mindu, Undali, Mtitu, Mirambo etc etc ndio utachoka kabisa.

Mambo ya Sq footage, financing etc jaribu kuperuzi websites za hawa 'wawekezaji.'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…