Mikopo ya ujenzi, kununua na kukarabati nyumba sasa inapatikana crrd mpaka 500mil.

Kitomai

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Posts
1,074
Reaction score
308
Sekta ya ujenzi wa nyumba imezidi kupata ahueni baada ya Benki ya CRDB kuzindua mkopo maalumu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba uitwao ‘Jijenge’, utakaokuwa mfumbuzi wa tatizo la changamoto zinazowakabili Watanzania katika ujenzi wa nyumba. Jijenge inatarajiwa kutatua tatizo la ujenzi wa nyumba, ununuzi wa vifaa vya ujenzi au ukarabati wa nyumba ambapo watu binafsi huwachukua hata miaka 10. Tofauti na mkopo wa nyumba wa awali uliokuwa ukilipwa kwa miaka mitano, mkopo wa Jijenge utalipwa kwa kipindi cha miaka 20, kwa riba ya asilimia 18 na asilimia 1 ya mkopo ikiwa ni kwa ajili ya bima. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei alisema wakati umefika kwa Watanzania kuishi maisha marefu ndani ya nyumba zao wenyewe kwa amani. “Kumiliki nyumba kunatosheleza hitaji muhimu sana la mwanadamu na kumpa heshima na utulivu wa fikra na maisha. Nyumba bora ni hitaji la muhimu kabisa kwa binadamu kama ilivyo chakula na mavazi. Jijenge pia itawahudumia wale watakaohitaji mkopo huo kwa ajili kukarabati nyumba,” alisema Dk Kimei. Kimei alisistiza kuwa mkopo huo utawafaa wafanyakazi wasio na kima cha chini ya 200,000, wafanyabiashara, wakulima na wavuvi, hata hivyo alibainisha kuwa ni nyumba 15,000 tu zinajengwa kwa mwaka tofauti na hitaji la nchi. Alisema kumekuwa na changamoto nyingi zinazokwamisha ujenzi nchini ikiwemo kupanda kwa gharama za kumiliki ardhi, gharama za vifaa vya ujenzi na kukosekana kwa mfumo thabiti wa kifedha wa kusaidia sekta hiyo.

Katika picha: Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo
 
Attachments

  • kimei.jpg
    kimei.jpg
    38.1 KB · Views: 354
  • juu 209.jpg
    juu 209.jpg
    263.4 KB · Views: 377
Nimepata hizo habari kupitia "e- statement " nikatamani kuuliza zaidi ila namba walizotoa hazipokelewi,
Hivi ni kweli sisi tuliojiajiri wenyewe tuna nafasi kwenye hiyo mikopo au ni marketing hype! , product nyingi za mabenki yetu zinawalenga walioajiriwa,
 
da yaan nliipania sana huu mkopo wa nyumba. nmefuatlia m city wakasema ukichkua 20M wanakukata zaidi ya laki 3 kwa miaka 20. nilipojaribu kupiga mahesabu nikajikuta kutakiwa kulipa zaidi ya 73M ss nikashindwa. Hii prog inawafaa wenye nazo tu na si maskini
 
Hv mbona wanatangaza intrest 18% lakin pesa wanazokata ni zaidi ya riba hiyo? Halafu wanakata bima ya mkopo ila ukimaliza kulipa deni hawarudishi hiyo pesa ya bima, au sera ya BOT inasemaje?
 
da yaan nliipania sana huu mkopo wa nyumba. nmefuatlia m city wakasema ukichkua 20M wanakukata zaidi ya laki 3 kwa miaka 20. nilipojaribu kupiga mahesabu nikajikuta kutakiwa kulipa zaidi ya 73M ss nikashindwa. Hii prog inawafaa wenye nazo tu na si maskini
Jaribu kupanua japo kidogo uwezo wako wa kufikiria, unajua kitu kinachoitwa "Time Value of Money"? Kwa lugha nyepesi, ulishawahi kufikiria miaka 20 iliyopita Shs. 500 ya leo ilikuwa na thamani gani kwa wakati huo? Kama huwezi kufikiria basi kamuulize Baba yako atakuambia. In the same way, hiyo 20m/= yako ya leo unadhani itakuwa na thamani gani miaka 20 ijayo, tena ukizingatia mfumuko mkubwa wa bei ambao Serikali ya M.k.w.e.r.e. imeshindwa kuudhibiti? Think Big pal!
 
Mkuu halafu hii time value ya money mbona mashirika ya hifadhi ya jamii hayaitumii hii manaake ukiweka pesa unakuja ipata ile ile hata ukijitoa baada ya miaka kadhaa,limekaaje hili
 
Wizi mtupu. Hawana nia thabiti wala ya dhati kumsaidia mtanzania wa kawaida. Kusudi ujenge nyumba ya maana inabidi ukope labda kuanzia 75M. Baada ya muda huo utatakiwa kulipa zaidi ya 250M. Not fair at all.
 
Mkuu halafu hii time value ya money mbona mashirika ya hifadhi ya jamii hayaitumii hii manaake ukiweka pesa unakuja ipata ile ile hata ukijitoa baada ya miaka kadhaa,limekaaje hili
Ni unyonyaji mkubwa, na bahati mbaya nchi tumewaachia wenye akili ndogo waongoze akili kubwa! Hakuna anayehoji maana sidhani kama hata akili zao zinatosha kufikiria haya. Wewe ulishawahi kuona wapi hela aliyokaa nayo mwenzako kwa zaidi ya miaka 30 anakuja kukurudishia kama ilivyo na kukudanganya na viji-benefits vya kipuuzi kama vile Maternity, Funeral Grant, Medical, Survivor, etc? Ukilinganisha alicho-invest na kuchuma kwa miaka yote hiyo na kile anachokupa ni sawa na anayepanda kilo 10 za mahindi halafu anakuja kuvuna magunia 150! Dah, ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
Jaribu kupanua japo kidogo uwezo wako wa kufikiria, unajua kitu kinachoitwa "Time Value of Money"? Kwa lugha nyepesi, ulishawahi kufikiria miaka 20 iliyopita Shs. 500 ya leo ilikuwa na thamani gani kwa wakati huo? Kama huwezi kufikiria basi kamuulize Baba yako atakuambia. In the same way, hiyo 20m/= yako ya leo unadhani itakuwa na thamani gani miaka 20 ijayo, tena ukizingatia mfumuko mkubwa wa bei ambao Serikali ya M.k.w.e.r.e. imeshindwa kuudhibiti? Think Big pal!

kweli kabisaaaa!
 
yaani mkuu yaani ....... amakweli viongozi wetu ni vipofu sijui wanawazaga nini manaake vitu nyeti kama hivi hawazungumzii sijui ni miradi yao.
 
Naomba kufahamishwa na yeyote mwenye kufahamu kuhusu ujenzi wa nyumba. Mil 20 kwa sasa unaweza kujenga nyumba yenye ukubwa kiasi gani na kiwango cha hiyo nyumba inakuwaje?
 
Jaribu kupanua japo kidogo uwezo wako wa kufikiria, unajua kitu kinachoitwa "Time Value of Money"? Kwa lugha nyepesi, ulishawahi kufikiria miaka 20 iliyopita Shs. 500 ya leo ilikuwa na thamani gani kwa wakati huo? Kama huwezi kufikiria basi kamuulize Baba yako atakuambia. In the same way, hiyo 20m/= yako ya leo unadhani itakuwa na thamani gani miaka 20 ijayo, tena ukizingatia mfumuko mkubwa wa bei ambao Serikali ya M.k.w.e.r.e. imeshindwa kuudhibiti? Think Big pal!

Likewise nyumba ya 20m ya leo in 20 years haitakuwa na thamani ya 20m
 
Jaribu kupanua japo kidogo uwezo wako wa kufikiria, unajua kitu kinachoitwa "Time Value of Money"? Kwa lugha nyepesi, ulishawahi kufikiria miaka 20 iliyopita Shs. 500 ya leo ilikuwa na thamani gani kwa wakati huo? Kama huwezi kufikiria basi kamuulize Baba yako atakuambia. In the same way, hiyo 20m/= yako ya leo unadhani itakuwa na thamani gani miaka 20 ijayo, tena ukizingatia mfumuko mkubwa wa bei ambao Serikali ya M.k.w.e.r.e. imeshindwa kuudhibiti? Think Big pal!
Mkuu usidanganye watu ukafikiri hawajui thamani ya pesa.
Interest rate ya mkopo kwa 18% ni wizi wa mchan, wakati inflation rate ni chini ya 7% leo hii.
Sasa hiyo riba ina cover risk gani na ni kwa nini.
No wonder mabenki karibu yote yana fedha ya kukopesha ambayo haina wateja.
 
Wadau huu mkopo ni majanga nilienda kuulizia kwanza kwa mtu ambaye take home ni kama milioni moja maxmum wanakupa milioni 15 tu na riba yake ni kubwa masharti ni haya.
1.lazima uwe na kiwanja chenye hati alafu watume valuer wao akafanye tathimin ya kiwanja ili ukishndwa kulpwa wakiuze na nyumba.
2.mfano wakikupa m15 hawakupi yote..a)wanakupa pesa ya msng wa nyumba kama m 4. Ukmalza msng wanakuja kufanya tathmni kama kweli ni cha m 4 dn b)wanakupa hadi lenter kama m 5. Then wanakuja kufanya evaluation kama kweli ni m5 umetumia,,c)wanakupa 7 kumalizia wanakuja kufanya evaluation mtanzania mwenye yuwezo wa kupewa milioni 500 ni yule anayelipwa kwa mwezi kuanzia milion 30 ambao hawazidi kumi nchi nzma
3.wengi wakishndwa kuzilipia either kwa kufukuzwa kazi au mikataba kwsha i.e mining sector...apo wananuza nyumba na land yako ni moja ya mikopo ya kinyonyaji...bora uchukue mkopo wako wa 20m ujichange kdogokdogo ifke ata 40 ujenge smple house si huu ambao unaatarsha ata kiwanja chako
nilifka crdb personly nikapewa dtail bt kjuujuu mtu akskia 500 anaoana ni easy task bt ni hatarai
 
Huwa nasikia kuna interest at reducing rate na interest at fixed rate hasa kwenye masuala ya mikopo. Ninaomba kujulishwa hizo terms mbili kwa huo mkopo wa tujijenge- crdb wenyewe wana rely kwenye lipi? Pia naomba atakayekuwa na majibu atufafanulie hizo terms mbili. Tunahitaji kufahamu mengi kabla hatujaamua kuchukua mkopo. Watoa mikopo hawaelezi kwa kina zaidi ya kukuambia interest yetu ni 18%. OMBI:
Ninaomba serikali itusaidie kuzungumza na wamiliki wa benki ili waingie mkataba na benk hata kama ni benk moja waangalie uwezekano wa kupunguza hiyo riba hata ikifika 10-12%. Ili kuwasaidia tabaka la chini ambalo ndiyo hasa hawana hata nyumba za kuishi waweze kumiliki hata vibanda vya kuishi.
 
Back
Top Bottom