mikopo ya vyombo vya usafiri ni ya wakubwa tu-hazina

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
hii ndiyo message niliyopata baada ya kuapply mkopo wa vyombo vya usafiri kwa wafanyakazi wa serikali.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
mikopo ya magari ,pikipiki au baiskeli kwa mujibu wa waraka wa serikali wa mwaka 2011.

Du kweli serikali yetu ni mufilisi yani wanashindwa kumkopesha mfanyakazi hata ka-corolla au hata ka-OPA? Hao wakubwa wanaowasema wana miili ya tembo au wana miguu 10?
 
Wa2 wengine wanapenda kuwalisha sumu wenzao tu, hiyo meseji uliyopata ni ni ipi?
 
Wa2 wengine wanapenda kuwalisha sumu wenzao tu, hiyo meseji uliyopata ni ni ipi?
meseji hii nimeipata baada ya mimi na wafanyakazi wenzangu kuufuatilia mkopo huo bila mafanikio.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
meseji hii nimeipata baada ya mimi na wafanyakazi wenzangu kuufuatilia mkopo huo bila mafanikio.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Labda hamna sifa! au mpo kenye list, ninavyofahamu wote walioomba awamu ya kwanza walishapewa fedha na tayari watumishi wameomba kwa awamu ya pili ndo wanasubiri. Naamini waraka uliuelewa vizuri usilaumu wasiohusika. Km wewe ni mtumishi wa serikali naamini utakuwa unaelewa namna taratibu za fedha zinavyochukua muda c km taasisi za fedha zinazotoa ndani ya saa 24, kuwa na subri mkuu na fuatilia kwa wakuu wako kwa ufafanuzi zaidi.
 
najua umeshtushwa sana na habari hii.
Najua unaelewa madudu mnayoyafanya hapo hazina.
 
Maneno ya mfa maji wewe una mikopo lukiki bado unataka kukopa, ndo maana huna sifa, jifanyie tathmini mkuu acha kulalamika.
 
hii ndiyo message niliyopata baada ya kuapply mkopo wa vyombo vya usafiri kwa wafanyakazi wa serikali.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Mkuu hii habari siyo kweli. Mbona mie nimepata. Ila mikopo yenyewe siyo mizuri kwani gari wanazokopesha ni mpya tu hivyo makato yake wengi hawawezi kulipa. Wangekopesha hata magari yaliyotumika. Nadhani mkuu kipato chako inaonesha hukopesheki. Kwani mie nimekopeshwa MITSUBISH HARD TOP 2500 CC kwa 51,705,120.00
 
Mafurahia watu wanaojitahidi kueleza ukweli, sa huyu jamaa keshamwaga sumu humu inywewe af ye anakaa pembeni, kumbe anajua hana vigezo, af sheriamya kununua 'used' nafkiri anajua serikali haiimind,
 
kuna mikopo ya magari mapya,magari used,spea za magari,pikipiki n.k
mikopo imegawanyika katika viwango tofauti kulingana na TGS yako.
Kwa kiwango ulichokitaja hapo juu inaonyesha wewe ndio sehemu ya wale wakubwa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Mafurahia watu wanaojitahidi kueleza ukweli, sa huyu jamaa keshamwaga sumu humu inywewe af ye anakaa pembeni, kumbe anajua hana vigezo, af sheriamya kununua 'used' nafkiri anajua serikali haiimind,

naona ulipost huku unasinzia!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Maneno ya mfa maji wewe una mikopo lukiki bado unataka kukopa, ndo maana huna sifa, jifanyie tathmini mkuu acha kulalamika.
ndio majibu yenu haya pale hazina.unataka kusema mkurugenzi alikuwa mwendawazimu kunipitishia ombi langu ?yaani hakuangalia kama nina makato mengine?kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Mkuu Mpigauzi nimependa ulivyochangia hoja kwa umahiri mkubwa, mimi pia ni mtumishi wa serikali kipato changu hakizidi milioni moja na nusu na wala hakipungui milioni moja kwa mwezi. Naomba ni-pm jinsi ya ku-apply hiyo mikopo/hatua za kupitia.

Maana kwenye idara yetu huo waraka tunausikia tu lakini wakubwa bado wameukalia, je nianzie wapi hapa hapa ua hazina moja kwa moja?
 
labda utueleweshe inaelekea unafahamu wa hiyo mikopo.je mtu akiaply inaweza chukua muda gani?na inasimamiwaje ili hadi wa chini wapate?
 
Jingalao, wewe unafahamu kabisa unadaiwa NMB, SACCOS na Bayport. Ni ngumu tu hata mtu wa kawaida kukukopesha siyo tu kutokukopesheka bali haukatiki!
 
labda utueleweshe inaelekea unafahamu wa hiyo mikopo.je mtu akiaply inaweza chukua muda gani?na inasimamiwaje ili hadi wa chini wapate?
Kwanza mikopo hii inatolewa kwa wafanya kazi wa serikali tu, wizara na idara za serikali na siyo Halmashauri.
Kila idara/kitengo kinakuwa kinapata mgao kulingana na bajeti iliyotolewa kwa mwezi husika, mkuu wa kitengo atatoa taarifa kwa watumishi ili wajaze fomu za maombi kwa kulingana na mgao, mikopo hiyo inatolewa kwa makundi kadhaa mf. mkopo wa samani, matengenezo ya gari/pikipiki, kununua gari lililotumika au gari jipya n.k
Sifa ya mwombaji ni lazima asiwe na mkopo unaoendelea au km upo akiomba kukopeshwa salio la mshahara(basic salary/take home balance) isiwe chini ya 1/3 ya mshahara wako basic.
 
Ahsante kwa ufafanuzi kamanda nimekupata.Je kuna wakati maombi yanakua pending kwa muda mrefu sana.au tunapigwa juu kwa juu na wakubwa.zetu.maana ukiwa mikoani hata kuambiwa zipo hawsemi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…