Mikopo ya wafanyakazi

AMARIDONG

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2010
Posts
2,501
Reaction score
185
Wadau naomba kuuliza kama kuna mtu anafahamu benki yoyote ambayo inatoa mikopo kwa wafanyakazi(personal loan)ambayo interest yake ni nafuu below 20.Sio lazima benk hata taasisi yenye masharti nafuu

tafadhali wakubwa
 
Waone NMB, Stanbic na ABC
Ila Stanbic ni wazuri kwa wafanyakazi iwapo wataingia mkataba na muajiri wako, utawafurahia.
 
Waone NMB, Stanbic na ABC
Ila Stanbic ni wazuri kwa wafanyakazi iwapo wataingia mkataba na muajiri wako, utawafurahia.
ahsante sana mpevu abc ni akiba au azania au nyingine
 
Nenda Twiga Bancorp. Wanatoa mikopo kwa wafanyakazi. Ila Stanbic wako vizuri zaidi.
 
Mkuu Malila Twiga Bancorp nao si ni lazima mkataba na mwajiri uwepo??

mana huwa kuna tatizo kwa upande wa waajiri wengine wanakuwa watata sana kufanya mkataba na bank kwa ajili ya wafanyakazi wake kupata mkopo.:disapointed:
 
Mkataba lazima uwepo,ila wao sio wasumbufu kama mwajiri wako ni mwelewa. Tatizo ni kwamba, bila mwajiri kuthibitisha kwamba wewe ni mwajiriwa wake na yuko tayari kwa lo lote,benki wataamini vipi?
 
Tambua kuwa TWIGA BANCORP ni ya serikali, na serikali yetu si unaijua jinsi ilivyokaaa. Wao kwao hata uki-sepa hawakufatilii sana shauri ya hali ya ufisad..., hiyo ndio advantage ya pale twiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…