Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,860
Hadi kufikia Machi 31 mwaka huu, Wizara ya Elimu ilihitaji kiasi cha Sh86.5 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wananfunzi, Bunge lilielezwa jana.
Mbali na kiasi hicho, hadi kufikia wakati huo, Serikali ilishatoa kiasi cha Sh1.75 trilioni kwa wanafunzi 293,765 kama sehemu ya mkopo ambao unajumuisha na wanafunzi 34,620 wanaoendelea na masomo yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama aliyesema fedha hizo ni sawa na asilimia 16.88 ya mikopo iliyoiva.
Mhagama alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la la msingi la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), aliyetaka kufahamu idadi ya wanafunzi waliokopeshwa kama wamepata kazi na wamemaliza kulipa mikopo yao.
Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani na wanafunzi waliokopeshwa, lakini hawajapata kazi baada ya kumaliza masomo yao ili waweze kurudisha fedha na ziwasaidie wengine.
Wanafunzi 34,620 walio katika kipindi cha matazamio ya mwaka mmoja na wanafunzi 163,281 ambao wamemaliza kipindi cha matazamio, wote ni sehemu ya wanufaika wa mkopo huu, alisema Mhagama.
Chanzo:Mwananchi