Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
MKOSI JUU YA MKOSI
1. Nimeenda zangu kunywa uji kwenye chimbo moja jipya ila kwa kuwa nilikuwa na wana ng'ambo ya barabara, nikaamua nibebe uji ili nikajumuike nao.
Mhudumu akaniambia bei ya uji ni mia tatu na kama nilitaka KUONDOKA na kikombe basi niache chenji, mfukoni nilikuwa na jero, lakini pia nilikumbuka nilihamia mtaani hapo siku mbili nyuma hivyo, sikuwa na sahani wala bakuli, sembuse kikombe!
Nimetoa jero, imebaki mia mbili, wakati bei ya kikombe kipya ni zaidi ya buku jero. Ulichowaza ndicho nilichofanya.
Naamka asubuhi siku ya pili, mama mwenye nyumba wangu ananiambia, "eh baba, ahsante kwa uaminifu, umeona uje na kikombe changu mpaka nyumbani baada ya muuzaji kufunga mapema." Nikamjibu asijali maana nilifunzwa UTU NA MAADILI, kimoyomoyo nikasema NIMEUMBUKA.
2. Nikaona ninyuke zangu shati jeupe na suruali NYEUSI na kwenda mjini kubahatisha. Kumbe wanafunzi wameruhusiwa kwenda kushiriki mahafali ya shule ya jirani. Kondakta akanitosa akisema " HAKUNA NAFASI KWA WANAFUNZI" Nilipojaribu kumweleza, akaniambia, " ndivyo mlivyo, WABISHI kama nini?" Kujichek vizuri, kumbe UFUPI HUU na vile nilivyovaa nilikuwa sare na wale wanafunzi.
3. Nikapokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa "shangazi yenu" ambaye ni Mroma.
Kumbe kanifanyia surprise, kawaambia wazazi wake kuwa mchumba wake alitaka awaone.
Kutokana na mabalaa ya konda na yale mavazi, si niliona nishai na kurudi mageto na kutinga "mtisheti, mjinzi na mkapelo"
Nikaanza mojamoja mpaka kwa "shangazi yenu". Vaa yangu ikawakata stimu wazee. Nikaambiwa si MAADILI kuvaa kofia. Loooh! Nilipovua wakauliza kwa pamoja, " MAJIVU YAKO WAPI???"
Nikajikanyaga nikidhani walimaanisha nilikuwa nakula ile kitu ya "JEMYEIKA"
Kuja kushtuka "TUUU LEITI"