Habari wadau? Jaman mie nauliza kama Ruaha panafaa kwa kilimo cha mbogamboga kama nyanya, vitunguu hoho na kadhalika. Nimepata shamba kijiji kimoja kinaitwa msolwa. Ni mbele ya hifadhi ya Mikumi kidogo. Maeneo ni mazuri wanalima mpunga,viazi vitamu na hata ufuta sometimes. Shamba nilolipata kuna mto usiokauka. Nimependelea kupanda mbogamboga kwa sababu barabara sio mbaya na maji ni ya uhakika so ntalima kwa timing ya soko. Tafadhalini nijuzeni wenye ufahamu wowote kuhusu hili tafadhali.