Mikusanyiko ya kidini yalaumiwa kwa kuenea kwa Surua Zimbabwe

Mikusanyiko ya kidini yalaumiwa kwa kuenea kwa Surua Zimbabwe

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Wizara ya afya ya Zimbabwe imesema Jumapili kwamba mlipuko wa Surua umeua watoto 80 nchini humo tangu Aprili, wakati ikidai mikusanyiko ya kidini imesababisha kuongezeka kwa maambukizi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wizara hiyo katika taarifa imesema kwamba mlipuko huo sasa umesambaa kote nchini na kusababisha asilimia 6.9 ya vifo miongoni mwa walioambukizwa. Waziri wa Afya Jasper Chimedza amesema kwamba kufikia Alhamisi wiki iliyopita, kulikuwa na kesi 1,036 zilizoshukiwa kuwa za surua, wakati 125 zikithibitishwa tangu kutokea kwa mlipuko huo.

Jimbo la Manicaland mashariki mwa Zimbabwe linasemekana kuongoza kwa maambukizi. Chimedza ameongeza kusema kwamba kesi ya kwanza iliripotiwa Aprili 10 na tangu wakati huo maambukizi yameenea kote nchini, yakisemekena kuchochewa zaidi na mikusanyiko ya waumini makanisani.

Wengi walioambukizwa ni watoto wenye umri kati ya miezi 6 na 15, wengi wakitokea kwenye familia za waumini waliokataa chanjo dhidi ya surua kutokana na imani za kidini. Baadhi ya madhehebu nchini Zimbabwe huwakataza wafuasi wao kupokea aina yoyote ile ya chanjo au matibabu. Madhehebu hayo yana mamilioni ya wafuasi wanaoamini miujiza ya uponyaji pamoja na kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

===========

Zimbabwe blames measles surge on sect gatherings after 80 children die

HARARE, Aug 14 (Reuters) - A measles outbreak has killed 80 children in Zimbabwe since April, the ministry of health has said, blaming church sect gatherings for the surge.

In a statement seen by Reuters on Sunday, the ministry said the outbreak had now spread nationwide, with a case fatality rate of 6.9%.

Health Secretary Jasper Chimedza said that as of Thursday, 1,036 suspected cases and 125 confirmed cases had been reported since the outbreak, with Manicaland in eastern Zimbabwe accounting for most infections.

"The ministry of health and child care wishes to inform the public that the ongoing outbreak of measles which was first reported on 10th of April has since spread nationwide following church gatherings," Chimedza said in a statement.

"These gathering which were attended by people from different provinces of the country with unknown vaccination status led to the spread of measles to previously unaffected areas."

Manicaland, the second-most populous province, had 356 cases and 45 deaths, Chimedza said.

Most reported cases are among children aged between six months and 15 from religious sects who are not vaccinated against measles due to religious beliefs, he added.

Bishop Andby Makuru, leader of Johanne Masowe apostolic sect, did not immediately respond to a request for comment.

In Zimbabwe, some apostolic church sects forbid their followers from taking vaccinations or any medical treatment. The churches attract millions of followers with their promises to heal illnesses and deliver people from poverty.

Source: Reuters
 
Chanjo ya surua ipo..wafanye kampeni ya kitaifa kuchanja watoto.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ile dini ya kina yuda ni shida kweli aisee wayahudi
 
Back
Top Bottom