Mikutano Mikuu ya Simba na Yanga haina tija

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Nimekuwa nikifuatilia sana mikutano mikuu ya vilabu vikongwe kabisa hapa nchini Simba na Yanga, mikutano inakuwa na mambo mengi na wakati mwingine ikibainika mkutano utakuwa wa moto wanasubiria timu icheze uwanjani ili wanachama wawe busy kwenda uwanjani.

Tena kuwafanya kuwa wajinga wanawapa kabisa tiketi bure ili wasipige kelele huku wakiwasindikiza na pilau au biriani.

Sasa najiuliza inakuwaje mkutano mkuu wa kujadili maendeleo ya timu wanachama hawapewi fursa ya kutoa michango au kujadili?

Mfano mkutano wa jana taarifa imewasilishwa ya mapato na matumizi kuwa klabu imetumia bilioni 17.3 out of 17.8, and 500 millions zimebakia.

Kuna agenda nyingine zimewasilishwa pale mkutanoni, its well and good, mbona sasa wanachama hawapewi nafasi ya kutoa ushauri, maoni, kuuliza pale penye wasiwasi, kueleza changamoto wanazoziona, naona mnaongea ninyi tu viongozi halafu sisi tunawasikiliza t, tena kutufanya mazuzu mnatutangazia kabisa kocha mpya pale pale ili tutoke kwenye mstari.

Haya mambo cjui ya kumleta Manzoki kwenye mkutano na kutufanya siso wajinga yataisha lini?

Kwann vilabu hivi vinakosa utawala bora, maana tenets za good governance ni participation, accountability, transparency and rule of law.Haya mambo ni muhimu sana ili vilabu vyetu viwe modern.

Kuendesha mpira kwa style ya marehemu Jimmy David Ngonya yamepitwa na wakati.

Wanachama amkeni, amkeni, sio mnasindikiza wenzenu kwenye utajiri tu.Vilabu hivi ni vya wanachama, hao wachache tumewachagua wafanye kazi kwa niaba yetu.

Mm nimeanza kwenda kuishangilia Simba enzi za winga mkimbiza upepo Sunday Juma, enzi za akina Juma Limonga, Adam Seleman, Aston Pardon, Mosses Mkandawile.Hawa akina Try Again hata kufikiria habari za Simba bado, Simba inamsajili Omary Hussein Kevin Keegan kutoka Yanga tunashangilia kutoka uwanja wa uhuru shamba la bibi tunaingilia chuo cha ualimu sasa hivi Duce tunatokea kwenye mnara wa ndege (kuna ndege iliwahi kuanguka pale uwanja wa mkapa kabla ya ujenzi wa uwanja wa mkapa) tunatokea shule ya msingi mgulani tukiimba Omary Hussein, Kevin Keegan.

Leo tunatoa ushauri wa namna ya kuboresha timu mnatudharau na kutuona mafala, nyie ndio mnajua sana, mimi tawala zote za Simba hadi waliokufa kwa kurogwa kwa sababu ya maslahi nipo Simba, kwahiyo I know the club very well.

BMT naomba mzibane hizi klabu mikutano yao iwe na tija na wanachama tupewe fursa ya kuhoji.Mkutano ambao hautaruhusu wajumbe kujadili uhesabike ni batili, hata kama wataweka watu wa kujadili lakn italeta sense.
 
HAYA NDIYO MAWAZO YA MASHABIKI TUNATAKA SIYO HUYO SHABIKI WA SIMBA GENTAMYCINE KILA KUKICHA YULE MCHAWI YULE MCHAWI.

BROO UMEANDIKA FACT SANA [emoji41][emoji123]
 
Yanga amewatoa panya shimoni.

Leo wanaona hakuna umuhimu wa mikutano mikuu kwasababu hii Bajeti ya Bil 20 imewaumiza walio wengi ambao hawajui hata ilipo ile Bil 20 ya uwekezaji.
 
Heti wanachama hawajapewa muda wa kuuliza maswali?

Looh Yanga inafanya. Watu waonyeshe makucha yao.[emoji1]
 
Haya mambo cjui ya kumleta Manzoki kwenye mkutano na kutufanya siso wajinga yataisha lini?

Mm nimeanza kwenda kuishangilia Simba enzi za winga mkimbiza upepo Sunday Juma, enzi za akina Juma Limonga, Adam Seleman, Aston Pardon, Mosses Mkandawile.Hawa akina Try Again hata kufikiria habari za Simba bado, Simba inamsajili Omary Hussein Kevin Keegan kutoka Yanga tunashangilia kutoka uwanja wa uhuru shamba la bibi tunaingilia chuo cha ualimu sasa hivi Duce tunatokea kwenye mnara wa ndege (kuna ndege iliwahi kuanguka pale uwanja wa mkapa kabla ya ujenzi wa uwanja wa mkapa) tunatokea shule ya msingi mgulani tukiimba Omary Hussein, Kevin Keegan.

BMT naomba mzibane hizi klabu mikutano yao iwe na tija na wanachama tupewe fursa ya kuhoji.Mkutano ambao hautaruhusu wajumbe kujadili uhesabike ni batili, hata kama wataweka watu wa kujadili lakn italeta sense.

WanaThimbaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yanga amewatoa panya shimoni.

Leo wanaona hakuna umuhimu wa mikutano mikuu kwasababu hii Bajeti ya Bil 20 imewaumiza walio wengi ambao hawajui hata ilipo ile Bil 20 ya uwekezaji.
Wewe unajua hiyo million 500 iliyobaki ilipo?
 
Yanga amewatoa panya shimoni.

Leo wanaona hakuna umuhimu wa mikutano mikuu kwasababu hii Bajeti ya Bil 20 imewaumiza walio wengi ambao hawajui hata ilipo ile Bil 20 ya uwekezaji.
Jibu hoja zake sio kurukaruka je wanachama walishiriki kutoa michango yao au walipuuzwa?
 
Back
Top Bottom