Mikutano ya Jumuia ya Afrika Mashariki sasa ni kiswahili tupu

Mikutano ya Jumuia ya Afrika Mashariki sasa ni kiswahili tupu

daza steven

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
359
Reaction score
358
Lugha hadhim ya kiswahili sasa inakamata kasi ya ajabu katika nyakati hizi Afrika na dunia kwa ujumla, wakati juzi ndani ya mkutano wa wabunge wa Afrika mashariki na wageni mbalimbali kutoka nchi za Africa waliudhuria kikao hicho cha kwanza kikubwa kufanyika cha aina yake na kutumia kiswahili mwanzo mwisho tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Julius Malema ambae alikuwa mmoja wa wageni kutoka Afrika ya Kusini yeye alikili kuwa sasa saa imefika waafrika tutumie kiswahili kama Lugha yetu ya biashara, elimu, kazi na mawasiliano, Malema alitumia neno AFRICA IDENTITY. MaLema ambaye ni kiongozi wa chama cha Upinzani cha Economoc Freedom Fighter (EFF) Nchini Afrika ya Kusin, alienda mbali zaidi na kusema kuwa yeye anajua maneno kidogo sana ya Kiswahili kwani alikuwa anawasikia kaka zake na baba zake ambao walikaa na kusoma Mazimbu na Dakawa kule Morogoro. Aliendelea kusema kuwa maneno mengi yanafanana na Kizulu kama Babu, Mama na mfundishaji ambapo wao wanatamka mfundisi.

Wabunge kutoka Uganda nao walisema kikao kilikuwa kizuri kwani walijikaza kusikiliza kiswahili kwa muda wote na kuchangia na kuhaidi kuwa sasa hawatakiita kiswahili lugha ya machokolaa kama walivyoaminishwa ukonyuma.
Ikumbukwe kuwa nchi ya Uganda hasa wananchi wake hawakipendi Kiswahili kutokana na dhana iliyojengeka miongoni mwao. kwani kiswahili kilikuwa kikitumika jeshini zaidi, magerezani na polisi na machokolaa ambao walikaa sana jela au asikari magereza.

Nchini Kongo ni tofauti kabisa na Uganda kule kuongea Kiswahili unaonekana ni mjanja tena unaakili na umetembea duniani. Niajabu sana ukiingia Kongo tena vijijini ndani ndani watu wanakigonga cha ugoko ugoko lakini wanaongea sana koswahili. Namtu akitaka kuonekana ni mtu wa watu atajitaidi kutumia kiswahili iliakubalike.

Kiswahili kimekuwa kikienea kwa kasi kubwa hasa neno la hapa kazi limekuwa likitumika katika mataifa mbalimbali duniani kama Brazil, Uingereza, Marekani na Asia.
Hadi sasa kiswahili kinaongelewa kwa wastani Omani 40% wanaongea Kiswahili, Afrika ya kusini, China, Marekani, Madagaska. Nchi zingine ni Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Kongo, Somaria, Zambia Malawi na Mozambiq kidogo sana.

Tayari hadi sasa radio zinazotumia kiswahili duniani ni Radio ya Kiswahili ya china, Idhaa ya kiswahili Ujerumani, BBC kiswahili, VOA Kiswahili Marekani, redio ya kiswahili Afrika ya kusini na zingine.

Na maraisi wanaoongea kiswahili vizuri ni Uhuru Kenyata wa kenya, Kabila wa DRC, Kriel wa Afrika ya kati na Raisi wa Zimbabwe anaitwa (Mamba) Mhs. Mnangwagwa. Hawa wote kwa nyakati tofauti walikaa sana Bongo na kujichanganya na wasahili.
Je, Kuna ubaya gani kujivunia Kiswahili ambacho ni kibantu na chimbuko lake ni Tanzania au nalo tuliweke katika Itikadi?

Mdau wa Kiswahili nchini.
Mzee Daza.
 
habari njema kwa watanzania
ushawahi kuona mtu mwingine anaongea broken english lakini aibu unaona wewe?
mmeshanielewa
 
Back
Top Bottom