Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Umri wa kuishi huchangiwa na maisha yako ya kila siku. Kuanzia vyakula, pombe, mazingira unayoishi kama ni sehemu yenye hewa safi utaepukana na magonjwa yanayoathiri mfumo wa upumuaji.
Kuna muandishi mmoja alisema maisha unayoishi yanatabiri maisha yako miaka kumi mbele. Maana yake kama wewe ni mtu wa kutembea hata masaa mawili kila siku iwe kwa kupenda au kwa kukosa nauli ya basi una uhakika miaka kumi ijayo utaweza kumudu matumizi ya miguu yako vyema tu. Kama ni mnywa konyagi chupa kila siku usishangae kupata matatizo ya ini miaka kumi ijayo.
Wale watu ambao culture zao haziruhusu kunywa pombe mara nyingi huwa wana umri mrefu zaidi ya walevi. Licha ya hayo wataalamu wanasema kunywa kwa moderation yaani glass moja tu ya 125 mils jioni kabla ya kulala inaweza kukusaidia kurefusha maisha.
Kuna wanaoomba kufa mapema kutokana na matatizo yaliyowazunguka na kuna wanaokufa mapema na kuacha ukwasi Iwan mali nyingi wala wasingemaliza kuzitumoa hata wangeishi miaka 200 duniani.