Milango ya kibiashara yafunguka Kenya na Tanzania baada ya kuondolewa kwa vikwazo

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Kuondolewa kwa Vikwazo 30 Kati ya 64 vya kibiashara baina ya nchi ya Tanzania na Kenya, kumechangia kufunguka kwa milango ya kibiashara katika Mpaka wa Namanga.


Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, Nurudin Babu.


Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, Nurudin Babu alifanya ziara katika mpaka huo aliwataka madereva hao kuzingatia usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Babu alisema mazungumzo ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wa Kenya Uhuru Kenyatta, kumeleta matokeo mazuri kwani kwa sasa mpaka huo magari ya mizigo ni mengi na mwingiliano wa kibiashara ni mkubwa sana.

"Kuwepo kwa mwingiliano huu ni fursa, hivyo baada ya wiki moja eneo la maegesho ya magari makubwa litakua limekamilika na halmashauri itaongeza mapato ya ndani kupitia maegesho hayo" alisema Babu.

Nipashe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…