Milion 3 biashara gani naweza kufanya?

Mama Derick

Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
33
Reaction score
1
Habari zenu wanajamvi!kabla ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa manajamvi kwa michango ya mawazo mbalimbali ambayo inatusaidia wengi wetu.
wana jf wamekua sio wachoyo wa mawazo na ama kwa hakika wa tz wote tungekua tunapeana michango na mawazo kama ivi,tungefika mbali sana.
Mimi ni mfanyakazi serikalini,mshahara ninaopata si mkubwa sana,nilikua nafkiria kujishughulisha na mradi ambao utanisaidia kidogo kusogeza ili gurudumu la maisha.Swali langu ni kwamba,nina 3 mil naweza nkafanya biashara gani?
Naomba mnisaidie mawazo yenu wakuu!
 
Mama Deric,
Ungependa uwekezaji wa muda mfupi nadhani kutokana na kusema ikuwezeshe kusukuma gurudumu la kila siku.

Je, Uko selective kwa biashara? Inategemea pia unakaa wapi....But nadhani unaweza fungua Genge, Ukaweka kijana akauza Matunda, Nyanya. Mboga mboga nakadhalika. biashara hii inaweza kuku cost china na 2million, and believe me Return ni kubwa ya kutosha.

But nahisi ukieleza unakaa wapi, Uko tayari kufanya white color business or huchagui yaweza kuwa rahisi kuchangia.
 
Kweli "USILOLIJUA NI USIKU WA GIZA", wengine wanatafuta Mitaji na huku wengine wanatafuta mpango wa kuanzisha biashara tu.

Bali naamini kupitia JF wengi wametoka gizani na tutaendelea kutoka gizani.

Mama Deric Kuhusiana na Biashara gani ufanye kwa mtaji huo; itategemea na ufahamu/ujuzi ulionao kwani mtaji huo unahitaji biashara ambayo msimazi wake wa karibu ni wewe mwenyewe. Ningekushauri kufuga ng'ombe wa Maziwa kama una eneo la kutosha.
 


hivi kwa joto la dar, ng'ombe wa maziwa ni biashara inalipa au ni ile kujisikia tu kuwa nimefuga ng'ombe wa maziwa? maana ngombe wa maziwa kwa ukweli wanastawi sana maeneo ya baridi.
 
Ingefaa zaidi kama ungetuambia ni biashara gani unafikiria kuliko kutokuwa kabisa na wazo ndio maana unaona michango unayopata ina maswali zaidi kuliko majibu unayotaka.
 
Mama Derick mbona hujibu hoja tutakusaidiaje sasa
 
mama derick... nunua boda boda mbili.... kila wiki hesabu ni sh.. 50,000x2=100,000....100,000x4=400,000

mwaka mmoja na nusu ni 400,000x18= TZSH 7,200,000

mode of operation...tafuta madereva wawili wazuri ingia nao mkataba kwamba wataendesha piki piki kwa miezi 18.. mwaka mmoja na nusu.... baada ya hapo piki piki zitakua mali yao kwa wao wenyewe kuzilipia pole pole ndani ya miezi hiyo 18 kwa kuleta hesabu ya wiki na kuilipia piki piki kwa kiasi cha sh. 55,500 kila mwezi kutoka kwenye mfuko wao au chanzo chao chochote cha kipato

at the end... TSH 7,200,000 kwa mwaka mmoja na nusu as returns.... na total of ths 1,000,000 @ boda bodax2= 2,000,000 as salvage value of your investment (boda boda).... jumla kuu ni TSH....9,200,000 ......ondoa 6,000,000 ....keep 3,200,000

buy another 4 boda boda for 6,000,000...... another one and half year your have 18,400,000 ...... so in three years

18,400,000 + 3,200,000= 21,600,000

21,600,000 ondoa 3,000,000 rudisha postal bank au yeyote aliyekuazima = baki kuu ni 18,600,000...

ukitaka kuendelea nunua piki piki nane..... .....!!!!!!!
 

maesabu mazuri sana tena sana kasoro ujaweka hesabu ya miguu na mikono ya bandia kwa madereva watakao tumia mwaka mmoja na nusu bado mda atakao kaa muhimbili na siku hizi hawakai sana mana wanakata miguu na mikono kupunguza garama za kuuguza
 

naishi songea kwa sasa.biashara ya matunda naona kama haitalipa uku kwa sabb upatkanaji wa matunda uku ni mdogo,matunda meng yanaagizwa nje ya mkoa
 

sina eneo kubwa sn apa kwangu.vp kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji?
 

nashkuru kwa mawazo yako mkuu
 
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana
 
Omba mungu apishie mbali majanga!!
 
We zinywe pombe tu, make hizo huwezi kufanya chochote. ukilazimisha kufanya biashara yoyote haziwezi kutoka make ni kidogo sana

Haya ndio mawazo finyu, nenda kariakoo wajasiriamali wadogowadogo ukawaulize! Watu walianza na 50,000 sasa wana zaidi ya 10 mil!
 
Fuga nguruwe kama imani yako inaruhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…