Milioni 10 za kila goli kwanini zisiwe zinapelekwa kwenye vituo vya watoto yatima?

Milioni 10 za kila goli kwanini zisiwe zinapelekwa kwenye vituo vya watoto yatima?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2023
Posts
1,483
Reaction score
2,392
Wadau nawasabahi,

Mada hapo juu inahusu Fedha anazotoa Rais kwa kila goli litakalofungwa na Vilabu vya Simba na Yanga kwenye Mashindano ya Kimataifa yanayoendelea.

Ni jambo zuri Mh. Rais analolifanya lakini kwa kuwa vilabu vya Simba na Yanga viko chini ya Wizara ya Michezo na Wizara ina Bajeti yake nilitarajia Fedha hizo zilipaswa zitengewe kwenye Bajeti kwani Ushiriki wa vilabu vya Tanzania unajulikana kuwa ni kila mwaka.

Pia TFF ina Fedha Inapata kutoka FIFA nadhani TFF ingetenga FEDHA kwa ajili ya kuhamasisha Vilabu kwa kununua Magoli kama anavyofanya Rais hivyo Fedha kutoka Bajeti ya Wizara + na Fedha kutoka TFF ndio zitumike kununua magoli ili zile MIL. 10 za RAIS ziwe zinapelekwa kwenye vituo vya watoto yatima na wale wanaoishi katika maisha magumu.
 
Eti kusafirisha mashabiki, upuuzi mtupu. Nchi ina changamoto kibao zinahitaji fedha hawajapeleka.
 
Back
Top Bottom