kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Benki ya Stanbic TZ imeingia makubaliano na Shirika la Kuhudumia Watoto (Unicef) kwa kutoa sh250 milioni, zitakazotumika kwa muda wa miaka mitatu kwa ajili ya kusaidia mradi wa WASH kwenyd shule za msingi za SERIKALI ili kupunguza magonjwa yatokanayo na hali duni ya maji na usafi wa mazingira.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Bodi ya benki hiyo, Hatibu Senkoro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa wanafarijika kuingia makubaliano SERIKALI na Unicef, kwa lengo la kuboresha maisha na tabia za baadaye za watoto kuanzia shule ya msingi kwa kupunguza kasi ya magonjwa ya tumbo.
"Mchango huu utasaidia kuboresha upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazinira kwa ajili ya shule tatu za msingi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, kwa wastani watoto 800 watanufaika katika kila shule," alisema Senkoro.
Source by: NIPASHE.
My take:
01. Je huu ni msaada au ni mkopo?
02. Na Je Kama ni mkopo' uwa SERIKALI inatozwa kiasi gani cha riba?
03. Na kwanini SERIKALI ikope fedha kwa ajili ya shule 3 tu? Wakati kuna shule nyingi za msingi zenye matatizo makubwa zaidi ya hizi?