Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 412
Baada ya kupitishwa na Bunge la Katiba (ambalo limejaa CCM) rasimu ya katiba itapelekwa kwa wananchi ili waipigie kura ya KUIKUBALI au KUIKATAA. Natumaini kwa wingi wa WATANZANIA (milioni 40+) dhidi ya CCM (milioni 6), ni wazi WATANZANIA wataikataa RASIMU ambayo itakuwa imechakachuliwa sana na Wabunge wa CCM. Sheria inasema baada ya kukataliwa na WATANZANIA, rasimu itarejeshwa tena Bunge la Katiba ili kurekebisha vipengele vinavyokataliwa na WATANZANIA . Baadae WATANZANIA NA CCM watapiga kura tena, na sheria haisemi IKATALIWE HADI MARA NGAPI NA NINI HATIMA YA KUKATALIWA MARA ZOTE.