Milioni 878.4 alizoidhinisha Rais Samia zimeboresha sekta ya mifugo nchini, vikundi 20 vyakabidhiwa madume ya ng'ombe

Milioni 878.4 alizoidhinisha Rais Samia zimeboresha sekta ya mifugo nchini, vikundi 20 vyakabidhiwa madume ya ng'ombe

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi David Silinde amesema katika kipindi cha miaka miwili tangu Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, serikali imenunua madume ya ng’ombe ya kisasa 366 yenye thamani ya Silingi Milioni 878.4 ili kuboresha mifugo nchini.

Silinde amebainisha hayo akiwa katika Kata ya Dakawa, Mvomero Mkoani Morogoro wakati wa hafla fupi ya kugawa madume 40 kwa vikundi vya wafugaji 20 ili kuboresha mifugo yao ya asili katika wilaya hiyo.

Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu amekuwa akifanya kazi nzuri katika kipindi kifupi kwenye Sekta ya Mifugo akiwa na lengo la kuinua wafugaji nchini kwa kuwa na mifugo bora na kisasa.
 
Back
Top Bottom