Milioni ngapi zinatosha kujenga nyumba hii!?

Milioni ngapi zinatosha kujenga nyumba hii!?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Wakuu salaam
Nipeni mchanganuo wa ujenzi wa nyumba yenye vyumba viwili na sebule chumba kimoja ni master
Na vyoo vya nje
Kwa hapa mwanza inaweza kucost sh ngapi?
 
Wakuu salaam
Nipeni mchanganuo wa ujenzi wa nyumba yenye vyumba viwili na sebule chumba kimoja ni master
Na vyoo vya nje
Kwa hapa mwanza inaweza kucost sh ngapi?
1. Inategemea na landscape (je unajenga kwenye sehemu tambalale, gentle slope au steep slope?).
2. Ukubwa/udogo wa vyumba vyako.
3. Quality ya finishing materials.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ukitaka kujenga usisubiri kuwa na mamilion kadhaa ndio ujenge

kama una kiwanja anza mdogo mdogo kwa awamu , chora ramani tafuta mafundi wa kawaida kama unawajua sio macontractors huko wapo bei ya juu wengine wanapiga kwa % ya material. utapata kiasi cha material yayohitajika na kadhalika.

mie naweza kukwambia itagharimu 20m kumbe 30m ukaanza kuchanganyikiwa na kujenga ni mipango mkuu
 
Dah..... Itakugharimu kuanzia 2m hadi 600m....
Uamuzi ni wako[emoji41] [emoji13]

Sent from my beretta ARX 160 using JamiiForums Mobile App
 
hongera mkuu kwa wazo lako la maendeleo, kama wadau walivyoshauri hapo juu kukadiria gharama juu kwa juu inawezekana na hapo nakushauri andaa (15m na kuendelea) kiulingana na ain a ya finishing utakayoitaka. ila kwa 15m unahamia kibishi( utakuwa umeweka paa la bati za kawaida, umeweka drill za madirisha na milango ya nje, na sometime umemwaga zege ndani ya nyumba). ila ukitaka gharama halisi kabisa zenye variation kidogo unaweza ni pm, kwa kua ni kazi inayohitaji muda kidogo na hakuna mtu wa kukufanyia free.
 
Kuna ramani ya nyumba ya bedroom 3 ,moja ikiwa master. INA public toilet .nilimuuliza injinia gharama ya nyumba kama hiyo ni bei gani .Jibu lake alisema ukiijenga kimaskini inaisha kwa 35 Milioni. Ukiijenga kawaida itagharmu 70 Milioni .Ukiijenga kifahari itaisha kwa Milioni 105. Kwa hiyo ukisikia MTU anakupa gharama kubwa sio kwamba anakutisha ispokuwa angalia nyumba yake ni ya kundi gani . mfano paa la mabati gauge 28 linaweza kula 25m kutegemea ni aina gani. Wakati paa la nyumba hiyo hiyo ukitumia Bati gauge 30 itachukua Milioni 4. Mfano tena hiyo nyumba ukiweka sakafu ya tiles za Spain itagharimu milioni 10 na sakafu ya simenti itakugharimu Milioni 3. Na zote ni nyumba usingizi unapata ule ule kutegemea Afya yako .gharama za nyumba zinaachana mno .La muhimu jenga kutokana na mfuko unavyokuruhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wazo kalitia mdau hapa lilikuwa lenyewe kuazia mil 5 na kuendelea maana inategemea unajenga nyumba ya aina gani.hata ya mil 5 unaeza jenaga kulingana na ulipo
Upatikanaji wa mafundi materal usafiri na land Scap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom