Milipuko ya gurunedi yakumba Bujumbura

Milipuko ya gurunedi yakumba Bujumbura

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Idadi ya watu wasiojulikana huenda wamejeruhiwa katika shambulio la gurunedi usiku wa Jumatatu katika mji mkuu wa kibiashara wa Bujumbura nchini Burundi.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema milipuko miwili mikubwa ilisikika baada ya gurunedi mbili kulipuka katika kituo cha mabasi kilicho na shughuli nyingi, Damu ilionekana katika eneo la tukio.

Wanasema maafisa wa polisi walifika haraka katika eneo hilo.

Milipuko miwili zaidi iliripotiwa , moja katika mtaa maaarufu wa Bwiza ambako guruneti ilirusha katikakati ya wauza samaki.

Mashuhuda wanasema kuna watu huenda wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa. Polisi hawajatioa tamko lolote kuhusiana na mashambulio hayo.

Hakuna kundi lolote lililojitangaza kuhusika shambulio hili lililotokea siku kadhaa baada ya Rais Evariste Ndayishimiye kusafiri New York ambako anatarajiwa kuhudhuria kikao cha 76 cha mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
 
Mashirika ya kuhudumia Wakimbizi wako kazini, Yale Mashirika hayako tiyari kuona Kambi zinafungwa kule Kigoma.
 
Kagame ana roho mbaya sana kama kimwili chake...

Nae huyu Rais wa Burundi wa sasa angejifunza kwa mwenzie ambaye hakutaka kusafiri nje kabisa, na alipojaribu kusafiri tu kuja TZ akapinduliwa, amshukuru sana Kikwete..
 
Back
Top Bottom