Millard Ayo unatakiwa ubadilike la sivyo utapoteza mashabiki ,Mambo ya clouds usiyachanganye na blogs zako

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Kwa muda mrefu nimekuwa nikimfuatilia huyu kijana na kweli amekuwa akivutia watu wengi kutokana na kipaji chake cha utangazaji, na millard ayo ametoka mbali sana hadi leo kufikia hatua kubwa aliyofikia

Kitu ambacho nimekiona na kama huyu kijana asipo badilika atapoteza mashabiki ni kutokana na kuendeshwa na clouds media hata kwenye media zake binafsi anazozimiliki, ikumbukwe kuwa Millard ayo anamiliki blog yake mwenyewe na Ayo tz, pia ana studio yake binafsi ya kisasa ambayo anamiliki yeye mwenyewe

Kinachomuharibia huyu kijana ni kitendo cha kutojiwekea masharti yake binafsi katika blog yake na ayo tv, Millard ayo amekuwa akiendeshwa na Clouds media hata kwenye kazi zake binafsi ambazo hazitakiwi kuingiliwa na clouds

Kwa mda mrefu imezoeleka kuwa clouds media ikiwa na mgogoro na mtu yoyote awe msanii au mtu binafsi basi millard nae amekuwa akifwata mkumbo na kuingiza migogoro hiyo kwenye media zake binafsi ambazo zina misingi yake isiyohitaji kuingiliwa

Tumeshuhudia mara nyingi clouds media inapojiingiza kwenye migogoro ambayo inaanzishwa na Ruge millard nae amekuwa akifwata mkumbo na kuliingiza hilo bifu hadi kwenye kazi zake binafsi kitu ambacho kinaweza kumuharibia kazi zake na kumpotezea mashabiki wengi wanaofuatilia blog yake na Ayo tv

USHAURI

mdogo wangu Millard napenda kukushauri tu ulipotoka ni mbali hadi hapo ulipofika, ni vyema ujijengee misingi yako kwenye media zako binafsi pasipo kuingiliwa na mtu yoyote la sivyo utajikuta unaendeshwa kijinga na kujikuta unapotea, Usiingilie migogoro ya clouds media ukachanganya na kwenye kazi zako binafsi utapotea

Zijenge Ayo tv na Ayo blog ziwe na misingi yake isiyoingiliwa na mtu yoyote, kama clouds wana bifu na mtu mwingine we achana nao, utakapokuwa kwenye amplifaya fwata masharti yao na utakaporudi kwenye ofisi yako binafsi na wewe uwe na misingi yako binafsi isiyo ingiliwa la sivyo utapoteza umaarufu kwani kinachokupa pesa nyingi ni views nyingi kwenye blog yako na ayo tv on youtube

Jijengee kujiamini ikiwezekana ni heri uachane na hao clouds ili uwe huru kabisa kwani now huna cha kupoteza clouds kwa hatua uliyofikia vinginevyo hao hao clouds watakuharibia kazi zako binafsi

Nawasilisha
 
Wewe unayetoa ushauri unamiliki hata blog? Mana unavyotoa ushauri kana kwamba upo kwenye industry ya social media, usitake kumchonganisha kijana na watu na clouds halafu baadae muanze kumcheka.
Wewe ni mpumbavu kabisa tena jinga inamaana hujui maana ya shabiki?

Sisi ndio tunmfanya aingize pesa kwa sababu ya mb zetu tunazopoteza online, hivyo tuna haki ya kumkosoa usiwe mjinga wewe
 
Mpaka sasa anaisoma namba na udenda unamtoka,maana habar za WCB na show za diamond alikua anapiga mpunga sanaaaa


SAMMISAGO ANAKUJA KWA KASI MAANA LICHA YA KUWA CHINI YA EATV,LAKINI HAINGILIWI BLOG YAKE NA HAO EATV.wanakwambia kufa kufaana banaa
 
You we'll said jamaa sasa hivi atarud kua chini ya blog ndogo,haoni kina globaltv online,dizzimonline,kina sammisago wanavosaka habar na bila kupelekeshwa hlvyo
 
Mpaka sasa anaisoma namba na udenda unamtoka,maana habar za WCB na show za diamond alikua anapiga mpunga sanaaaa


SAMMISAGO ANAKUJA KWA KASI MAANA LICHA YA KUWA CHINI YA EATV,LAKINI HAINGILIWI BLOG YAKE NA HAO EATV.wanakwambia kufa kufaana banaa
Yani wcb ndio ilikuwa inamuingizia pesa kupitia video zao ,bila kusahau drama zao zilikuwa zinampa views nyingi sana millard kwenye youtube kitu ambacho kilimuingizia pesa nyingi sasa anaanza kujiingiza kwenye migogoro ya kijinga atapotea
 
You we'll said jamaa sasa hivi atarud kua chini ya blog ndogo,haoni kina globaltv online,dizzimonline,kina sammisago wanavosaka habar na bila kupelekeshwa hlvyo
Jamaa atapotea mapema tu kwa kujiingiza kwenye migogoro ya clouds, alitakiwa awe na misingi yake binafsi isiyoingiliwa na mtu yoyote
 
Wewe ni mpumbavu kabisa tena jinga inamaana hujui maana ya shabiki?

Sisi ndio tunmfanya aingize pesa kwa sababu ya mb zetu tunazopoteza online, hivyo tuna haki ya kumkosoa usiwe mjinga wewe
Wewe kama nani bana unapayukaa
 
kesho utashangaa akilalamika uhuru wa habari unaminywa na serikali,kumbe hajui hata bosi wake anaminya uhuru wake wakuposti kitu chochote kile.Ila mcheki mwenzake Sam Misago,yy anarusha matukio yote tena kabase zaid katka entertainment bila kubagua
 
kesho utashangaa akilalamika uhuru wa habari unaminywa na serikali,kumbe hajui hata bosi wake anaminya uhuru wake wakuposti kitu chochote kile.Ila mcheki mwenzake Sam Misago,yy anarusha matukio yote tena kabase zaid katka entertainment bila kubagua
Kabisaa
 
HATERS VP BANAA,MBONA UMEZUKA NA JILIPOVU HIVYOOO.WACHA JAZBA MZEE.kwan kasema uongo hata akiwa njiwa
Wewe humpunguzii Millard ayo chochote kile huo Ushauri aliyeandika angefikiria ajiingizie vipi na yeye pesa watanzania tunapenda sana kufuatilia mambo ya watu ndo maana wazungu wanatuacha mbali sana kama anaona Millard ayo hapost angetumia fursa kuja na Blog yake aangalie afanye nini cha kumzid Millard hapa hakuna utimu bali unaelezwa ukweli kwa facts
 
Mm nilikuwa mpenzi mno wa millardayo, kiukweli sasa hivi ule mvuto wa miaka miwili nyuma wa millard ayo umepungua kiasi fulani, kuna watu humu walishamshauri hapunguze video kwenye habari zake na leo mkuu amemshauri atemane na mkumbo wa clouds, kujikwaa kupo ajicheki asimame aendelee, walaji wa mapishi yake ni sisi akubali kukosolewa tu,
 
Reactions: cdc
Wewe nawe ni jinga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…