KERO Millennium Tower 2, Lifti tano hazifanyi kazi inayofanya kazi ni lifti moja unaweza kusubiri zaidi ya dakika 20

KERO Millennium Tower 2, Lifti tano hazifanyi kazi inayofanya kazi ni lifti moja unaweza kusubiri zaidi ya dakika 20

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Nimeshangazwa leo nilipokwenda jengo Millennium Tower 2, kwa ajili ya suala la kiofisi, mjengo ambao unamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) nimekuta lifti tano zimefungwa hazifanyi kazi inayofanya kazi ni moja tu licha ya jengo hilo kuwa na ghorofa zaidi ya 25 ambazo utegemea miundombinu ya lifti kufika sehemu husika.

Kutokana na uwepo wa lifti moja inayofanyakazi, nimeshuhudia watu tukisubiri lifti kwa zaidi ya dakika 20 huku wengine wakidai wakati mwingine ikitokea lifti hizo zinatumiwa na wahudumu wa jengo hilo lenye kumbi za mikutano na ofisi, mfano kupeleka huduma kwenye kumbi wanaweza kukaa hata nusu saa wakiisubiti lifti moja.

Hali hii imenipa mashaka sana nimejiuliza maswali yasiyokuwa na majibu, kwamba lifti hizo mpaka zinaharibika kwa wakati mmoja wahusika walikuwa wapi? Je, kuna usalama wa kutosha kwenye hiyo 'lifti' moja inayotumika kwa sasa? Maana miezi kadhaa iliyopita watu kadhaa walijeruhia na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kupata matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo hilo.

Nashauri mamlaka husika zifuatilie kwa kina kama kuna uzembe wahusika wawajibike kwa kuwa hali hiyo itafanya baadhi ya kumbi na miundombinu nyingine ya kibiashara kutovutia kibiashara kutokana na changamoto hiyo hali ambayo inapunguza mapato.

Nimeambiwa jengo hilo limekuwa licha ya kumilikiwa na PSSSF lakini limekuwa likisimamiwa na Ms. Prolaty Ltd.

IMG_20240326_102234_618.jpg

Pia soma - Wasimamizi Millennium Tower 2 wakiri changamoto ya lifti, waomba watumiaji kuwa wavumilivu marekebisho yakiendelea
 
Nimeshangazwa leo nilipokwenda jengo Millennium Tower 2, kwa ajili ya suala la kiofisi, mjengo ambao unamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) nimekuta lifti tano zimefungwa hazifanyi kazi inayofanya kazi ni moja tu licha ya jengo hilo kuwa na gorofa zaidi ya 12 ambazo utegemea miundombinu ya lifti kufika sehemu husika.

Kutokana na uwepo wa lifti moja inayofanyakazi, nimeshuhudia watu tukisubiri lifti kwa zaidi ya dakika zaidi ya 20 huku wengine wakidai kuwa kwa wakati mwingine ikitokea lifti hizo zinatumiwa na wahudumu wa jengo hilo lenye kumbi za mikutano na ofisi, mfano kupeleka huduma kwenye kumbi wanaweza wamekuwa wakikaa hata nusu saa .

Hali hii imenipa mashaka sana nimejiuliza maswali yasiyokuwa na majibu, kwamba lifti hizo mpaka zinaharibika kwa wakati mmoja wahusika walikuwa wapi? je, kuna usalama wa kutosha kwenye hiyo 'lifti' moja inayotumika kwa sasa? maana miezi kadhaa iliyopita watu saba walijeruhia na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kupata matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jingo hilo.

Nashauri mamlaka husika zifuatilie kwa kina kama kuna uzembe wahusika wawajibike kwa kuwa hali hiyo itafanya baadhi ya kumbi na miundombinu nyingine ya kibiashara kutovutia kibiashara kutokana na changamoto hiyo hali ambayo inapunguza mapato.

Nimeambiwa jengo hilo limekuwa licha ya kumilikiwa na PSSSF lakini limekuwa likisimamiwa na Ms. Prolaty Ltd.View attachment 2945247View attachment 2945246

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Hii ndio rangi yetu halisi wabongo kwenye 1 na 2.

Usimamizi, utunzaji wa vitu ni hovyo kabisa
 
Tumo hapa kampuni za lift Bora Tanzania, ujinga ni kwamba wanapeana tenda ki mjomba mjomba, acha tuone kwanza
 
Gharama ya kuendesha majengo marefu ni kubwa sana. Lift, pump za maji, mastandby jenerators nk nk.
 
Back
Top Bottom