1973 RAJ MINJA
Member
- Aug 28, 2009
- 7
- 1
Mwanafunzi wa kidato cha nne aliyechaguliwa kujiunga chuo cha ufundi veta kibaha kongowe kafukuzwa chuo kwakuwa amekutwa na mimba hewa baada ya kwenda kupimwa katika zahanati ya kongowe. Hakuna kipimo kilichofanyika zaidi ya kuminywa matiti . Kawaida kipimo cha mimba kipo ni strip ya urine for pregnancy test hiki hakikufanyika pale zahanati ila walirubuniwa na pesa kidogo kumuandikia ripoti ya uongo kwamba ana mimba.
Kwa uchungu familia ya binti huyu walitafuta msaada kwa m.kiti wa zahanati ile hawakupata msaada, wakaenda kwa m.kiti wa serikali za mitaa bila mafanikio, haikutosha diwani kaelezwa naye kashindwa. Masharti wanayopewa kutoka kwa mwalimu mkuu baada ya kwenda kujieleza viongozi hao, anasema walete taarifa za daktari aliyempima akithibisha hakuwa na mimba ili aendelee na shule. Wakienda pale zahanati ya kongowe wanasema ili nao waandike hivyo vyema kwanza wakubali kama alikuwa na mimba ndipo wabatilishe,kwakuwa binti na wazazi wake japo si wasomi wanaelimu ya kujua kama wanarubuniwa hawakuweza kusaini hiyo karatasi.
Wanajamii wazazi wa huyu binti ni wakulima na uwezo wao ni duni wameshindwa wafanye nini au waelekee wapi? Wanasema ukielimisha mtoto wa kike ume elimisha jamii, je tunakwenda wapi kielimu kuhusu watoto wa kike. Huu ni uuwaji kabisa. Tunaomba msaada wa kimawazo hata wa kisheria. Imeniuma nimeleta kwenu jamii nanyi mchangie juu ya hili. ushahidi na vielelezo wa vipimo vilivyo pimwa hospitali tatu tofauti vipo vikionyesha hakuna mimba kwa siku ile iliyoonyesha ana mimba pale zahanati ya kongowe. Kwa tetesi nafasi amepewa mtoto wa kigogo kwa kuhonga laki nne.
Huyu mwalimu hafai na hapo zahanati huyo daktari hafai.
Viongozi wa serikali waliwajibishwa, kwanini na hawa waliohusika kumuharibia binti huyu wasishitakiwe kwa kosa hilo pamoja na mkuu wa shule?