Poluyakhtov
JF-Expert Member
- May 9, 2017
- 358
- 300
Habarini za usiku ndugu zangu,
Mimi ni kijana wa miaka 27, nimeoa miezi mitatu iliyopita. Sasa, juzi ghalfa mke wangu akaanza kujisikia maumivu upande wa chini wa kulia. Baada ya kumpeleka hospitali nikaambiwa ana UTI na Fangasi,alipewa dawa za kutibu hayo maradhi lakini hakupata nafuu.
Ikabidi nimpeleke tena Clinic moja akapate kipimo cha Ultra Sound.
Matokeo yameonesha kuwa ana Ectopic Pregnancy kwenye Ovary ya kulia.Sasa nimeshauriwa kumpeleka hospitali ya rufaa kwa msaada zaidi. Changamoto iliyopo ni kwamba kwa sasa kipato hakija kaa sawa(mimi ni mtu wa mshahara)na sijalipwa pato langu la disemba.
Ninahitaji kukopa fedha ili niweze kumsaidia mke wangu,lakini sijajua ni kiasi gani inagharimu kufanya hiyo operation kwa hospitali za serikali.Naomba kwa anayejua gharama zake anijulishe ili nijue nakopa kiasi gani na niweze kumsaidia.Asanteni.