Mimba imenifanya nichukie kuoga

Yaani naoga basi tu ili iwe mradi. Nimetokea kuyachukia kabisa maji ya kuoga.

Ambaye amewahi kukutana na kadhia hii anajulishe alivukaje? Mimba ina wiki 10
Sasa wiki 10 hiyo ni mimba? Kwl siku hizi hakuna wanawake, hapo bado atakavyomtesa kijana wa watu!
 
Kwa hiyo umeamua ukimbilie ChatGPT kuchukua ya kuandika , 😂😂
 
Yaani naoga basi tu ili iwe mradi. Nimetokea kuyachukia kabisa maji ya kuoga.

Ambaye amewahi kukutana na kadhia hii anajulishe alivukaje? Mimba ina wiki 10
Wewe ni mvivu tu wa kuoga hilo halina shaka

Watu wanasingizia sana mimba imemfanya hivi au vile napenda kuwaambia kuwa mimba haimfanyi mtu kitu ukijikuta uko na tabia furani jua ndivyo ulivyo

Iko hivi binadamu wote tuna conscious mind na unconscious mind Tabia nyingi hufichwa kwenye unconscious mind sasa mimba inapoingia inasababisha hormonal imbalance hivyo tabia uliyoificha inaibuliwa na kwa kuwa utasingizia mimba unajipa tumaini kuwa mimba imesababisha hakika mimba haisababishi bali inaibua tabia yako uloificha

Kwa mfano wote binadamu tuna tabia mbaya ambazo huwa tunazikandamiza zisionekane wazi kwa watu lkn wewe unaijua na unaweza ikandamiza mpaka ikawa haionekani tena hata wewe ukajishangaa na kujipa tumaini kuwa tabia hiyo haipo tena 🤣 huko ni kujindanganya tabia ipo na ikitokea kichocheo inaamka upya

Mfano mwanamke alikuwa anamzimikia jamaa furani kabla ya mimba akipata mimba anaweza mpenda jamaa huyo mpaka hatoweza jizuia hii inatokea na wanawake kwa uongo wao wanasingizia mimba 🤣🤣🤣🤣🤣 wapendwa hiyo haipo jua ulimzimia jamaa tu kabla ya kitambi cha muda

NB msisingizie mimba tena hizo ni tabia zenu malaika ameiweka live ujione ulivo
 
Aliyekupenda kabla ya mimba akipata mimba anakupenda zaidi hawezi jizuia

Anayekuchukia ila anajibaraguza kabla ya mimba akipata mimba atakuchukia live bila chenga utaona chuki yake 😂 halisi

Mimba haileti tabia ina ibua tabia ulizozificha ambazo ni tabia zako halisi 🤪🤪🤪🤪🤪
 
anhaaaa kumbe, ahsante mkuu umenipa mwanga angarau nimejua ABC
 
Tumewaacia mabwana kama mabinti na viherehere vyao na visebengo. Wanajuuua wanawake kuliko wanavyojijua wenyewe. Huwa nasoma comments nasema hiiiiii

Ps: sijasoma comments za hii thread
mwandko wako unaniumiza macho mkuu.

Nimesoma kwa kurudia coment yako ila sijaelewa umemaanisha nin
 
Ngoja niichukue hii namba moja😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…