mimba kwa mke wangu, na mimi nalamba malimao

g4cool

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
429
Reaction score
206
habari wana jamvi, mke wangu ni mjamzito wa kama miezi mitatu na nusu hivi, cha kushangaza na mimi nimeanza kupata hali ya kupenda vitu vya ajabu, nachagua chakula, napenda sana malimao na nimepata hali ya kupenda chocolate za dairy milk, nimepoteza hali ya kufanya kazi, ila kwenye mzigo nagonga kama kawa, hii ni nini?
 
mimba hiyoo mkuu hauna cha kushangaa hapo msaidie mkeo bana yy atamalizia tu kwenda labour
 
hahaaaa, duh.
Hii kali. Sijawahi kuisikia. Ngoja wataalam waje wakusaidie.
 
Afadhali we unalamba malimao, kuna mdau mmoja alikua anakula udongo na akawa anatembea mwendo wa paka
 

ndo maana ya kusaidiana katika hali zote,mume wangu alikua anatapika mpaka anakoma
 
hahaaaa, duh.
Hii kali. Sijawahi kuisikia. Ngoja wataalam waje wakusaidie.

hii ipo sana mkuu,wanaume wengi linawakumba,wengine hadi uchungu wanaumwa
 
Mie wakwangu kuamka kwenda kazini ni balaa yaani ni uvivu tu.
 
Kwa kiswahili fasaha hio hali ulokuwa nayo inaitwa UCHE na inawatokeaga baadhi ya wanaume pindi ambapo wake zao wakiwa wajawazito.Usiwe na shaka utarudia hali ya kawaida mkeo akijifungua...:smile-big:
 
heeh!! mpaka ajifungue tena?? yan nnakoelekea nahisi naweza acha kwenda kazini au kukosa baadhi ya siku coz nimekuwa mvivu balaa
 
Nimeisikia japonica sijakutana na sababu za kisayansi.....nahisi ni Suala la kisaklojia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…