Wanaume hawabebi mimba...unawezaje kubleed ikiwa wewe ni mwanaume?
Tarehe za kubleed haziwezi kukusaidia sana kwani zinabadilika. Cha muhimu kujua ni urefu wa mzunguko wako wa mwezi, yaani ni jumla ya siku ngapi toka unapoanza kubleed hadi unapobleed tena. Hiyo ndio starting point ya calender method of contraception.
Kwa hiyo range ya tarehe ulizotoa, ina maana mzunguko wako ni wa kati ya siku 28 hadi 30, ambao ni mzunguko wa kawaida kwa wanawake wengi.
Kwa kawaida yai (la kike) hutolewa siku ya kati kati ya mzunguko, kwa mzunguko huo wako...ina maana yai litatolewa siku ya 14 au 15 tangu ulipoanza kubleed. Mbegu (za kiume) zinaweza kuishi mpaka siku 3 zinapomwagwa ukeni, kwa hiyo basi..inabidi kutoa siku hizo 3 hapo tangu siku yai litoke (14 - 3 = 11), na yai huwa linakaa kwa siku 4 mpaka 5 kwenye mrija (fallopian tube) ambapo linaweza kurutubishwa, kwa hiyo basi..inabidi kujumlisha siku hizo 5 tangu siku yai litoke (14 + 5 = 19).
Kwa hiyo kama mzunguko wako ni wa siku 28 hadi 30, siku zako za hatari ambazo unaweza pata mimba ukifanya ngono zembe na kumwaga mbegu ndani ni kuanzia siku ya 11 tangu uanze kubleed, hadi siku ya 19 tangu uanze kubleed.
NB: Njia hii haikukingi na HIV, na nadhani HIV ni tatizo kubwa zaidi kuliko mimba....tumia condom, itakuepusha na yote!