ndugu, dadako anaimba kwaya na amepata mimba, au una maana gani kuleta thread hii hapa? mimba za makanisani ni chache sana kuliko za mitaani, makanisani watu mnaona kama ni kitu cha ajabu, na kweli ni cha ajabu, lakini ya mitaani inaonekana kama ni kitu cha kawaida ndio maana hata kuipublicise haihitajiki...upo hapo kulichafua jina la kanisa au? kwasababu kwenye makanisa ujue huwa kuna watu waliokomaa kiroho na wasiokomaa kiroho, wale wanaomjua Mungu kikwelikweli hawawezi kufanya hivyo, ila wale ambao wameokoka karibuni au wanaigiza, ndo huwa wanaleta sifa mbaya kama hiyo...may God help you.