Kama tukianza mjadala wa mimba za wanafunzi kwangu mimi ambaye ni mwalimu kitaaluma naona ni dhana paana sana, nina mifano migumu ya kuwatetea watoto na wazazi kwa wakati mmoja hivyo kuifanya mada kuwa ngeni na tata; kwa upande wa kwanza ni dhahiri kuwa kama tunataka kuweka suala hili vizuri basi tungetenisha mimba za wanafunzi kutokana na mazingira halisi maana kwangu mimi mimba za wanafunzi wa Dar ni tofauti kabisa na mazingira ya mimba wanayopatia mimba wanafunzi wa Kijijini kwetu Rangwi-Lushoto yaani ( Rural Vs Urban) ukiangalia fasta fasta (nimekuwa mwalimu kwenye shule za dar) utagundua kuwa mimba nyingi ( sio wote) kwa mjini husababishwa na tamaa waliyonayo watoto wenyewe; Mfano: nikiwa mwalimu wa darasa wa form four kwene shule fulani nilipata kushuhudia wanafunzi wakisisitiza kuwa wanataka wapate wanaume watakaowapatia simu, pesa ya chipsi, vocha na nguo na hivyo wamewaweka kataka category tofauti kulingana na mahitaji yake; hali hii huwaweka katika mazingira hatarishi ya Ukimwi na mimba. Wakati wale wa vijijini huweza kupata mimba (sio wote) kutokana na mazingira magumu kule wanakoishi; Mfano shule moja ambayo iko kilometa zaidi ya 100 kutoka Lushoto mjini kuelekea Kwekanga haina umeme, miundo mbinu, makazi hafifu, haina walimu, hakuna nyumba (hostel) za wanafunzi hasa hao wa kike na hivyo kujikuta wanafunzi wengi wakipangishiwa vyumba kwenye makazi ya watu, kumbuka sana; wanapangishiwa vyumba na wazazi wao lakini wakati huo huo wazazi hawa hawana uwezo wa kuwatimizi mahitaji yao ya kila siku hivyo kuwaacha watoto hawa wajiweke kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kuolewa wakiwa kwenye nyumba hizo za kupanga, na hii si Lushoto tu ni pamoja na shule za Mkoa wa pwani-Chanika, Lindi, Rufuji, Shinyanga-Bariadi.
Kwa mfano; last year nikiwa Bariadi nilifikia guest (hotel) fulani ambapo niliishi hapo kwa muda wa wiki moja na hivyo kuzoena na baadhi ya wahudumu wa pale, jambo muhimu hapa ni mhudumu mmoja ambaye kwangu alionekana kuwa na uelewa zaidi ya mambo na hivyo kunivutia nihoji elimu yake, binti huyu kwa uchungu alisema alipata mimba akiwa kidato cha pili na kwamba haikuwa kusudi lake bali ni tokeo la sababu kama nilizoeleza hapo juu, hivyo kurudi nyumbani na kujifungua salama na baada ya hapo alitamani sana kurudi shuleni lakini tayari nafasi ya kusoma haikuwepo tena na shida zilipozidi nyumbani aliamua kuondoka kuja Bariadi kutafuta kazi na kuangukia kuwa mhudumu wa gesti.
Mifano ninayo mingi inayoeleza maisha magumu ya wanafunzi wetu yanayopelekea kupata ujauzito lakini pia nisiache kugusia nafasi ya wazazi katika hili pia nalo ntalieleza kwa mfano; last year nikiwa mwalimu kwenye shule fulani hapa Dar, binti mmoja aliondoka nyumbani kwao na kwenda kukaa kwa mwanaume kwa zaidi ya wiki na kwa wale wanaokumbuka niliweka tangazo hapa jamvini na pia ITV walitoa tangazo kama hilo la binti kupotea nyumbani kwao, baada ya binti kurudi nyumbani na kuja kuripoti shuleni, shule ilitaka maelezo ya kina toka kwa wazazi na binti mwenyewe cha kushangaza wazazi hawakuonyesha ushirikiano na walimu na jivyo kuondoka na binti yao ) je katika mazingira kama haya utegemee nini?) lakini pia ushuhuda nilioupata toka kwa mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo 2010 katika mazungumzo yetu alikri kusema kuwa yeye ameachiwa na wazazi wake afanye anavyotaka kwa masharti kwamba akipata mimba asiipeleke nyumbani tu (so kinachofanyika badala yake ni arbotion) na kwa taarifa zaidi ni kwamba wanafunzi hawa ni mabingwa wa sehemu na aina za vidonge vya kutolea mimba!
Vipi bado niendeleeee, ngoja nifanye kazi za watu kwanza, ila naona kuna haja ya kuwa na mdahalo wa wazazi na wanafunzi kuhusu future ya watoto na kwamba hii ifanywe collectively na sio upande mmoja tu, ukienda au kama utafuatilia habari za watoto hawa zinatisha saaaana; Habari ya mwisho ni hii; last month mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne katika shule niliyokuwa nafundisha alitoroka kwao kwa lengo la kwenda kwa mwanamme wake lakini kabla ya kuanza safari yake ya kumfuata huyu jamaa mkoani; aliamua kupitia Sun Siro (sp) ili kujirusha na kesho asubuhi apande basi aondoke, akiwa ndani club akakutana na kijana na wakawa kampani, akapatiwa kinywaji na cha kushangaza alijikuta asubuhi akiwa gesti na akiwa ameshafanywa vya kutisha, just imagine form four last month, yaani ukifuatilia sana haya mambo utalia au utachanganyikiwa. Duh vidole vinauma ngoja nipumzike