Nimesoma comments zote.
Nilichogundua ni kwamba wengi waliochangia hapa (and probably jamii ya watanzania kwa Kiujumla) wanachukulia matatizo ya ujauzito kijuu juu. Hali hii ina uhasiana na vifo vingi vya vichanga na wazazi.
Kupitiliza tarehe ya kujifungua ni kiashiria cha hatari. Ni LAZIMA mjamzito anayejali afya yake, ya mtoto wake na ya familia yake kiujumla afanye jambo sahihi anapoona kiashiria cha hatari.
Katika hali kama hii jambo sahihi ni kufika kwa mtaalam kwa ushauri wa kitaalam.
Tuepuka tabia ya kuchukulia mambo kirahisirahisi kwa sababu kuna taarifa nyingi zinahitajika kabla ya kufanya maamuzi ya ushauri sahihi unaomfaa mjamzito kama huyu.