Pole sana ndugu kwa tatizo hilo la shemeji? Ni ujauzito wa ngapi? kama si wa kwanza tatizo kama hilo lilishawahi kutokea kwenye mimba nyingine? Ujauzito una umri gani?
Huduma ya kwanza; Akiwa amelala, hatakiwi kuinuka ghafla na kusimama inabidi akae kwa dakika takriban moja na nusu ndio asimame.
Endapo atapata dalili za kushuka presha inambidi akae au alale chini mara moja la sivyo ataanguka.
Mpe mchanganyiko wa glucose/sukari na chumvi kwa ratio ya 6:1 vikiwa vimechanganywa na maji.
Waweza kumpa glasi moja ya Fanta ikiwa na kijiko kimoja cha chumvi (tea spoon).
Mshauri aanze kwenda clinic (ANC) kwa ajili ya kuonana na wataalamu, na kushughulikia mwenendo mzima wa afya yake na huyo mtoto aliye tumboni.
Mara nyingi dalilli hizi zinasumbua kuanzia wiki ya 28 ya ujauzito na by 32 weeks huwa zinaisha kabisa. Baba unatakiwa kumpa support sana mkeo kipindi chote cha ujauzito kwani tafiti zinaonesha kwamba dalili nyingi hupungua kwa akina mama ambao waume zao wako pamoja nao psychologically. Jitahidi kumpa vyakula vya kujenga mwili na kuongeza damu na pia anywe maji ya kutosha.
Nakutakia kila laheri.