Mimba na Ujauzito

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Naomba mnijalie tofauti ya haya maneno
 
Ujauzito ni ule Uzito unaokujia... Mimba ni pale mtoto anapoanza kutungwa...
 
Ujauzito ni neno la kitafsida tu ila maana ni moja.

Mfano:
Mavi - Kinyesi
Kuzaa - kujifungua
nk
 
Mimba ni kwa wanyama na ujauzito ni kwa mwanadamu ila asilimia kubwa ya watu wanatumia mimba kwa mwanadamu.
 
Mimba ni kwa wanyama na ujauzito ni kwa mwanadamu ila asilimia kubwa ya watu wanatumia mimba kwa mwanadamu.

huenda utujalie ni kwa nini? mimba ni kwa mnyama?
 
nadhani mimba ni pale KE anapogundua kuwa haoni siku zake tena kwahiyo tunaita ana mimba kwa mwanzoni ila ujauzito ni pale tumbo linapokua kubwa tayari kwa mama kujifungua NDIO MAANA HUWEZI KUSIKIA MAMA MWENYE MIMBA BALI MAMA MJAMZITO. Ni mawazo tu wadau.
 
Ni tafsida tu kama mdau mmoja alivojibu hapa.

Mfano chooni - msalani nk
 
aiseeeeeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…