CHE_BUEVARA
Member
- Aug 11, 2021
- 5
- 3
Mambo vipi mwanajukwaa? Hivi una mdogo au mtoto wa kike? Sasa huu ndio wakati wa kumuwaza huyo binti yako aisee, wamombo wanasema ‘Imagine’ yani unaweza hata kufumba macho na kumvutia picha binti yako mwenye umri chini ya miaka kumi na tano (15) anatembea tembea hapo sebuleni kwako na kitumbo ‘ndii’ huku mkono wake mmoja kashika kiuno na mwingine una limao akijaribu kukata kile kichefuchefu na kisirani cha mimba changa.
Sasa hicho kitumbo ndio wataalamu wanakiita mimba ya utotoni na huku mtaani Bwana Roma aliyejichimbia zake Zimbabwe alituzawadia kibao chenye mistari “Gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto”. Ukweli ni kwamba, hizi mimba za utotoni zinatajwa kuwa miongoni mwa tatizo kubwa katika jamii za kitanzania ambalo hukatisha ndoto za wasichana wengi wadogo na kuingia katika maisha mapya tofauti na matarajio yao, wazazi wao na jamii kwa ujumla.
Wadau mbalimbali wa kutetea haki za wanawake na watoto hawapo nyuma katika kufanya jitihada za kufanikisha tunatokomeza kabisa tatizo hili na kuifanya jamii ya kitanzania kuwa ni mazingira salama kabisa kwa mtoto wa kike na ndoto zake. Moja ya hatua iliyoonekana kufanikiwa ni kushinikiza vyombo vya sheria ambavyo ni Mahakama na Bunge letu tukufu kupitia na kufanya mabadiliko katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 na 17 inayoruhusu binti mwenye umri wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi wake.
Sheria imejaribu kutanabaisha vitu vingi sana humo ila sasa kama wewe ulisoma darasa la saba ‘B’ kama mimi lazima uchanganyikiwe kwasababu, mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na nane (18) anatajwa kuwa ni mtoto na kuna sheria zinakutia hatiani kabisa ukijihusisha na uhusiano wowote wa kimapenzi na huyo mtoto.
Lakini sasa Dah! Wahenga walisema “Ya ngoswe, muachie ngoswe” hivyo nayaacha jamani hayo mambo ya vifungu vya sheria wenye taaluma yao wasije kunikalia kooni bure maana unaweza kuta nimekosea hata kunukuu. Haha! Lakini umekunywa maji leo? Maji ni uhai ndugu yangu, haya kunywa maji tuendelee sasa.
Hapa kuna maswali nataka tujiulize, Je! wasichana hawa wadogo wana taarifa sahihi kuhusu hicho kinachopiganiwa? Wapi taarifa sahihi kuhusu elimu rika na afya ya uzazi hupatikana kwa urahisi na njia rafiki zaidi kwa watoto wetu hasa wa kike ambao ndio wahanga wa tatizo hili? Wewe kama mzazi au mlezi umewahi kuzungumza na mdogo au mtoto wako wa kike kuhusu haya mambo ya afya ya uzazi? Kama bado jipige kifuani na ujisemee safari bado mbichi mnoo.
Tunashuhudia mara kadhaa kunaandaliwa kampeni na warsha mbalimbali zenye lengo la kuelimisha juu ya athari na jinsi ya kuepuka mimba za utotoni. Ni ukweli usiopingika kwamba washiriki wengi wa matukio haya huwa ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kusahau kundi la wazazi ambalo ni muhimu zaidi katika kupunguza na kumaliza tatizo hili la mimba za utotoni.
Mimi sijawahi kuona hizi warsha zimefika kijijini kwetu kwa kweli, yani hapo nimezisemea hizi ambazo nimeanza kuziona kwenye runinga tuu ila tuache hayo.
Wazazi wengi bado wana dhana potofu ya kutozungumza na watoto kuhusu elimu rika na elimu ya afya ya uzazi kwa ujumla, wakiamini kufanya hivyo ndio kuruhusu mtoto kujihusisha na masuala ya ngono moja kwa moja yani wanaona kama watamtamanisha mtoto kwenda kujaribu na kusahau kwamba kuna wajinga wapo huko nje wana msemo wao “Ukisubiri embe liive sie twalila na chumvi”.
Majukwaa rafiki ya elimu rika huandaliwa mara kwa mara na imekua sehemu ya vijana kuzungumza kwa kujiamini na kuhoji bila hofu juu ya utatuzi wa changamoto wanazokumbana nazo kila siku. Najaribu kuwaza matokeo ambayo tungeyapata ikiwa nyumba watokazo vijana hawa zingekua ndizo majukwaa rafiki zaidi kwa kupata elimu hii na wazazi ndio wangekua viongozi wa mijadala ya mambo mbalimbali kuhusu elimu ya afya ya uzazi.
Mawazo yakanipeleka mbali zaidi, nikakumbuka mapinduzi makubwa ya teknolojia ambayo kila siku vinavumbuliwa vitu vipya na nikajisemea vipi simu ambazo karibu kila mtu anamiliki siku hizi ikiwemo hao watoto tusiojua hata wanatumia vipi hizo simu zao zingekua ndio sehemu ya kuwakumbusha na kuwaeleza wazazi namna bora ya kuzungumza na vijana wao? Naamini ili tuweze kuuvunja mduara huu lazima tufanye jambo ambalo halikuwahi kufanywa kabla.
Upatikanaji wa taarifa hizi muhimu kiganjani sio tuu utasaidia mzazi kujifunza wakati wowote apatapo nafasi bali utapunguza gharama za uandaaji kampeni, matamasha na majukwaa mengi ambayo hukosa hadhira hii muhimu katika kuishinda vita hii.
Au basi tuseme haitopunguza gharama bali itaelekeza gharama sehemu ambayo ni sahihi zaidi kuwafikia walengwa wengi kwa wakati na kila mmoja kwa muda wake anaoona unamfaa kupata taarifa hizo. Ujue watu hawapendi kupangiwa, Hahaha!
Taarifa sahihi na zitakazopatikana kwa njia rafiki zaidi kuhusu elimu ya afya ya uzazi ndio mwarobaini wa tatizo la mimba za utotoni ikiwa mzazi atafanywa kuwa rafiki wa kwanza wa mtoto na kupewa elimu jinsi ya kuzungumza vyema na mwanae, hivyo kuvunja mduara wa upatikanaji na upashanaji finyu wa taarifa baina ya mzazi na mtoto.
Kabla sijaondoka hapa binti yangu ananikumbusha ule wimbo wa injili una mistari inasema “Ibada njema inaanzia nyumbani” lakini pia tusisahau mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi na huko nahisi ndipo ulipotoka ule msemo “Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu” na hapa ndio tunasema bora wali maharage kuliko walimwengu. Hahah! Asante kwa kunikaribisha. KAZI IENDELEE!

Upvote
1