Mimba ya Aunty Lulu yachoropoka baada ya kuangushiwa kichapo kikali cha mbwa mwizi na mpenzi wake...

Mimba ya Aunty Lulu yachoropoka baada ya kuangushiwa kichapo kikali cha mbwa mwizi na mpenzi wake...

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
ILE mimba ya miezi mitano aliyokuwa nayo staa wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ imechoropoka kufuatia kipigo alichopewa na mpenzi wake.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
auntylulu.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]




Sosi wa karibu na mwigizaji huyo, amenyetisha habari kuwa, mwanaume huyo (jina kapuni) aliyedaiwa kuwa ndiye mwenye ujauzito huo ambaye maskani yake ni Kinondoni, jijini Dar, alimshushia kipigo Aunty Lulu kwa sababu ya kumuonea wivu kwani amekuwa akimzuia hata kuongea na simu.

Sosi huyo alizidi kutiririka na sentensi kuwa, kutokana na kipigo hicho, Aunty Lulu aliumia na kuanza kuvuja damu kisha akakimbizwa hospitali kwa Dokta Mvungi (Kinondoni) ambapo aliambiwa mimba imeharibika na kulazimika kusafishwa kizazi.

“Vikao vya kumsema mwanaume huyo kwa kosa alilofanya vilifanyika nyumbani kwao Jumapili ambapo aliahidi kutorudia tena na kuomba radhi huku akiahidi kumfanyia makubwa Lulu,” alisema sosi huyo makini.

Baada ya paparazi wetu kuzinyaka habari hizo, alimwendea hewani Aunty Lulu, alijibu kwa unyonge na kusema ndoto zake za kuwa na mtoto zimeyeyuka kufuatia kipigo hicho.

“Sina la kusema zaidi, ndoto za kuwa na mtoto zimeyeyuka mwanaume huyu amezidi wivu lakini sina jinsi kwa sababu ndio baba mtoto na ameshaomba msamaha,” alisema Lulu.
 
Sense dogodogo center akabebe bure mmija
 
Hahaaaa kaona wa Tanzania ni watu wa kudanganywa kirahisi hivyo enhee. Ametoa mimba kwa hiari yake sasa anaficha aibu. Anajua kipigo cha kusababisha mimba kutoka hahaaa
 
Hivi lini hawa watu watatulia na kufanya mambo muhimu kuendeleza Tanzania
 
Hahaaaa kaona wa Tanzania ni watu wa kudanganywa kirahisi hivyo enhee. Ametoa mimba kwa hiari yake sasa anaficha aibu. Anajua kipigo cha kusababisha mimba kutoka hahaaa

huyu mimba zote anasingizia kipigo. kashatoa sana nahis afya yake si salama ndio maana anazitoa .

yani hanasikitisha kweli
 
Ntarudi baada ya muda kuna uzi wako 1 naenda kuutafuta ule uliweka picha za celebrities wenye mimba nakumbuka nliuliza km ma-Dr wapo kwny mgomo wa kutoa mimba?yametimia ntarudi mpwa.
 
By McDonaldJr

Duh ma-Dr wapo kwny mgomo au?kuna manguli hapo kati yao vp tena?

Zimekataa kutokaaa ndio maana wameamua wazae tuu,lakin Belina ashawahi kuolewaa au?
white girl uko wp swahiba njoo uku kwa jirani zile hbr zimeanza ss nahic mgomo wa ma-Dr umesitishwa.
 
Last edited by a moderator:
Zimekataa kutokaaa ndio maana wameamua wazae tuu,lakin Belina ashawahi kuolewaa au?
white girl uko wp swahiba njoo uku kwa jirani zile hbr zimeanza ss nahic mgomo wa ma-Dr umesitishwa.

Tulijua hata hivyooo et imechoropooka bila kuchokonelewaa lol hayaa na umri unaaendaa labda watazalia mbinguni
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom